Ijumaa, 25 Machi 2016

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee


Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na wazee wa mkoa wa Dare s Salaam walipokutana katika kikao ofisini kwake (Katikati) ni Mwenyekiti wa baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali na kulia ni katibu wa wazee hao  Mohamed Mtulia.
Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali akizungumza katika kikao cha wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto).
Katibu wa  wazee wa Dar es Salaam Mohamed Mtulia (Kulia) akizungumza wakati wa kikao  Mhe. Ummy mwalimu (kushoto) na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu(Kulia) akionesha kitabu cha sera ya wazee ambayo inatarajiwa kuandikiwa mswaada wa kuwa sheria na kupelekwa Bungeni kushoto ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.

Kaimu kamishna Ustawi wa Jamii Rabikira Mushi akizungumza katika kikao cha wazee wa Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Dar es Salaam Bi. Mary Chipungahelo(maarufu kama mama Chips) akichangia mada katika kikao kati ya baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
 Serikali imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.

Mpango huo umetolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam alipokutana nao mapema wiki hii ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. amesema wazee wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.

“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bunge mwezi Septemba ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza masuala yahusuyo wazee” Alisema Mhe.Ummy.

Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.

Aidha Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.

Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli  kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee nchini.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni