.

.
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 4 Oktoba 2017

UWT KYELA YAADHIMISHA MIAKA 39 , KWA KUTOA MSAADA KWA WAFUNZI YATIMA 35 !!

Mmoja kati ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ngonga iliyopo kata ya Ngonga katika halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya akikabidhiwa sare za shule pamoja vifaa vingine vya masomo!!


Katika kuadhimisha miaka 39 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) iliyo chini ya Chama cha Mapinduzi CCM, Umoja wa Wanawake wa CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wakiongozwa na mwenyekiti wao Bi. Rhoda Mwamunyange,

Ijumaa, 7 Julai 2017

MANISPAA YA ILALA YATOZWA FAINI KWA KUSHINDWA KUHUDUMIA DAMPO !!


NA:  EVELYN MKOKOI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akionyesha jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema hii leo jijini Dar es salaam ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Wilaya ya ILala.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akiwa ameambatana na Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi ambap ameipiga faini ya milioni 25 Manispaa ya Ilala kwa uchafu wa mazingira kwa wakazi wa Pugu.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akizumgumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo aliyoifanya katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Ilala jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akibadiishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema(katikati), Sophia Mjema na kushoto ni Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita wakati wa ziara ya ukaguzi wa uchafuzi wa mazingira uliofanyia katika dampo la Pugu KInyamwezi jijini Dar es salaam. 


Kufuatia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, iliyofanyika Jijini Dar es Salam leo katika Manispaa ya ilala, ilohusisha ukaguzi wa Dampo la Pugu Kinyamwezi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupitia Mkaguzi wa Mazingira wa kanda ya Mashariki Bw. Jaffari Chimgege, limeitoza faini Manispaa  ya jiji ya Dar es Salaam kiasi cha shilingi Milioni 25, kwa kosa la uchafuzi wa Mazingira wa kutohudumia Dampo hilo ipasavyo na kupelekea harufu mbaya, vumbi na maji yenye sumu kali  na kuhatarisha afya ya wakazi wa maeneo jirani viumbe hai na mzingira kwa ujumla.

Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Viwege uliyopo katika kata ya Majoe yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bi Amina Rashid yaliyoeleza kuwa na changamoto mbali mbali katika dampo hilo zikiwemo za vumbi na maji yenye kemikali kwenda katika maeneo ya makazi, Naibu Waziri Mpina, ameitaka Halmashauri ya jiji kuja na mpango mkakati utakaoweza kuupunguzia mzigo dampo la Pugu ambalo kwa sasa linatumika kupokea takataka zote za Halmashauri za jiji la Dar es Salaam na kuonekana kulemewa na mpango huo uwezeshe kila manispaa kuwa na dampo lake.

Aidha Mpina alibaini kuwepo kwa madhaifu makubwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kuondosha taka katika manispaa za jiji na kuutaka uongozi wa jiji Hususan Mkurugenzi wa Jiji kufuatilia madeni hayo kikamilifu, pamoja na kutoa deadline ya uwasilishwaji wa fedha hizo “ni vyema ghahama za uondoshwaji wa taka zikatokana na taka zenyewe na siyo kutoa fedha za kuhudumia taka kutoka katika vyanzo vingine vya mapato. Alisisitiza Mpina.”
Mpina pia aliitaka manispaa ya jiji  kutafuta namna bora ya kuondosha taka sumu na kuelekeza taka zote za matairi katika jiji la Dar es Salaam zitafutiwe sehemu tofauti na namna pekee ya kuzitekekeza.

Akionekana kuongea kwa hasira na msisitizo Naibu Waziri Mpina alisema, “ Hakuna kitu nisichopenda katika utendaji wangu kama kuona taasisi za serikali zikiwa za kwanza katika suala zima la uchafuzi wa mazingira, faini hiyo jiji mtailipa ndani ya siku 14, na kuhakikisha mnarekebisha  matobo yote yanayolalamikiwa kupitisha maji na kupeleka katika makazi ya wananchi pamoja na kujenga mifereji ya maji ya mvua, na maji ya sumu yaende katika mkondo sahihi wa maji hatarishi na bila kusahau kuruhsu maji hayo baada ya kujiridhisha na vipimo vinavyotakiwa.

Awali akitoa taarifa ya hali ya mazingira  na usimamizi wa taka katika Dampo  la Pugu Kinyamwezi , Mkuu wa Idara ya usimamizi taka wa jiji la hilo Bw. Shedrack Maximillian alimueleza Mpina kuwa jiji linakabiliana na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja dampo kupata moto, dampo kutokuwa la kisasa na maji yenye sumu kwenda katika makazi ya wananchi.

Hata hivyo Manispaa ya ilala imetenga kiasi cha fedha shilingi Bilioni moja za kitanzania kwa mwaka wa fedha ulioisha pamoja na kuzungumza na wadau wa maendeleo ikiwa ni mkakati madhubuti wa kuweza kuboresha Dampo hilo kinalotumika kwa kiasi kikubwa na manispaa zote za jiji la Dar es Salaam.

Alhamisi, 18 Mei 2017

"Polisi jijini Arusha wakana kuwasomba waandishi na karandiga, wadai waliwapa Lift"

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Claud Gwandu

Katika hali ya sintofahamu mapema leo jijini  Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia kusanyiko la watu walioongozwa na mstahiki Meya wa jijji la Arusha Kalisti Lazaro Bukhay,  kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba katika  ajali uliyopoteza uhai wa dereva, walimu na Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Jumatatu, 19 Desemba 2016

BANDARI YA DAR ES SALAAMA KUKOSA REKODI ZA TAKA NI UDHAIFU MKUBWA- MPINA

NA EVELYN MKOKOI – DAR ES SALAAM
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Viongozi wa Bandari ya Dar es salaam mara baada ya kuwasili Bandarini hapo kwaajiri ya kufanya ziara.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mzingira Mhe. Luhaga Mpina amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es salaam ili kujionea utaratibu wa Bandari hiyo wa kuondosha taka zitokanazo na shughuli zake.

Ziara ya Naibu Waziri Mpina imetokana na Malalamiko ya wananchi yaliyodai kuwa uchafuzi mwingi umekuwa ukifanyika katika Bahari na sehemu kubwa ya fukwe ya bandari imekuwa ikijaa taka za aina mbali mbali.

Kutokana na malalamiko hayo ya wakazi wa jiji la Dar es Saalam, Naibu Waziri kabla ya kukagua maeneo ya kutoa na kukusanya taka za aina mbali mbali katika bandari hiyo zikiwemo taka za mafuta ghafi, alipokea taarifa kutoka kwa uongozi wa Bandari ambapo ameshangazwa na kile kilicholezwa na Afisa Mazingira wa bandari Bwana Thobias Sonda kuwa Bandani hiyo kubwa katika kanda ya Afrika Mashariki haina sehemu ya kupokea taka yaani waste reception facility na haina takwimu za taka zinazoingia na kutoka Bandarini Hapo.

Akishindwa kujibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Naibu Waziri Mpina Afisa mazingira huyo alieleza kuwa, Bandari hiyo inazalisha aina mbili kubwa za taka ikiwa ni taka za aina mbali mbali na taka za maji taka, alisema kuwa taka hizo zinaondoshwa na wakala ambao wanasajiliwa na Sumatra lakini haikueleweka wazi kuwa, taka hizo zinatupwa wapi na aliongeza kwa kusema kuwa, taka nyingi na hali ya uchafu inayoonekana pembezoni mwa Bandari ya Dar es Salaam inatokana na shughuli za kibinadamu kiwandani hapo, na kusema kuwa, kuna utaratibu wa kufanya usafi na kuziondosha na kukanusha kuwepo kwa taarifa za boat na meli zinazofanya safari za kuanzia bandarini hapo kuchafua mazingira ya bandari na Bahari.

Afisa Mazingira huyo, liongeza kwa kusema kuwa taka za maji taka pamoja na kukosekana kwa takwimu za uondoshwani na umwagaji, zimekuwa zikikuswanywa na magari yao maalumu na kumwagwa katika mabwawa yao yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

Kwa kushangwazwa na hali hiyo, Mpina kupitia Baraza la taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC ameutaka uongozi wa Bandari hiyo kujenga mfumo mzuri wa kuhifadhi taka kwa muda wa miezi sita na kuripoti kwa Baraza za Mazingira kwa miezi mitatu Mfulizo kuonyesha namna ambavyo uondoshaji wa taka hizo unafanyika, Pamoja na kuwasilisha ripoti kwa Baraza ya  Namna ambavyo mawakala hao walipatikana.

Aidha Naibu waziri Mpina ameliagiza baraza kumpelekea ripoti  ndani ya siku saba, inayoonyesha kama hao mawakala wa kukusanya taka bandarini wapo kisheria.

Kwa Upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Nchini Bw. Nelson Mlele amesema kuwa amepokea maagizo ya Mhe kupitia NEMC kwani yanawakumbusha utekelezaji wa majukumu yao na kwa upande wa Bandari ni changamoto itakayofanyiwa kazi haraka.

Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya limemuondoa madarakani mwenyekiti wake kutokana na kukosa imani nae!!!


Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya leo limefanya kikao cha kuadhimia kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ndg. Alex Julius Kinyamagoha kwa madai ya kukosa imani nae baada ya mwenyekiti huyo kuandika waraka na kuusambaza katika mitandao ya kijamii Facebook na WhatsApp .

Katika waraka huo Ndugu Alex Kinyamagoha anadaiwa kuandika waraka unaopinga mabadiliko yaliyojadiliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa sanjari na kuwakashfu mwenyekiti CCM Taifa aliemaliza muda wake madarakani Ndg, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mwenyekiti CCM Taifa aliyopo madarakani sasa Mh. Rais John Pombe Magufuli na kuusambaza katika mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wake wa Facebook na Whatsapp mnano tarehe 15/12/2016.

Akizungumza katika mkutano huo ndg. Frank Boaz ambae ni mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa amesema kuwa kitendo alichofanya Alex Kinyamagoha kinaashiria dhahiri kuwa alitumwa hivyo chama cha CCM hakiwezi kamwe kuwavumilia mamluki kwa namna yoyote kwani shirikisho litajengwa na wanachama wenye nia njema hivyo shirikisho halitasita kuwaondoa mamluki na tayari shirikisho hilo limeanza na Alex Kinyamagoha.

Naye Katibu wa Siasa na Uenezi Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya ndg. Oddo Aidan Ndunguru, amesema kuwa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya limekerwa na waraka huo na ambapo aliwataka watanzania waupuuze waraka huo na watambue kuwa waraka huo ni mawazo binafsi ya ndg Alex Kinyamagoha na si Shirikisho kwani Shirikisho halijawahi kufanya kikao cha kujadili mabadiliko yaliyo pendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Hata hivyo akatumia nafasi hiyo kuwaomba radhi viongozi wote wa CCM na ngazi zote, wanashirikisho na wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi kote nchini ambapo alisema kuwa Shirikisho hilo linaunga mkono mabadiliko yaliyojadiliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na uteuzi wa viongozi uliofanywa.

“hakuna haja ya kuendelea kuimba CCM iyena iyena wakati mapenzi yako yapo nje ya chama hivyo ni bora ukatoka ukaenda huko ambapo una mapenzi napo, lazima tutambue kuwa kama watangulizi wetu wangefanya makosa CCM isingekuwepo leo hivyo ccm haita wavumilia mamluki kwa namna yoyote ni lazima watoke”.

Nduguru akamaliza kwa kusema nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya juu Mkoa wa Mbeya itakaimiwa na Ndg. Michael Malegesi hadi hapo uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo utakapo fanyika, na kwamba shughuli zote za Shirikisho zitaendelea kama kawaida.

Ikumbukwe kuwa Ndg. Alex Kinyamagoha aliandika waraka huo na kuusambaza katika mitandao ya kijamii Facebook kupitia ukurasa wake na WhasApp mnamo tarehe 15/12/2016, na manamo tarehe 16/12/2016 majira ya 11:51 usiku akaomba radhi kwa waraka huo katika mtandao wa kijamii wa facebook kupitia ukurasa wake uliosomeka kama ifuatavyo...



Aliekuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya.

Katibu wa Siasa na Uenezi Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya ndg. Oddo Aidan Ndunguru.

Frank Boaz Mjumbe akizungumza katika mkutano huo.

Michael Malegesi Kaimu Mwenyekiti Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, akizungumza katika mkutano huo

Jumamosi, 17 Desemba 2016

Mbunge Sugu "sikukimbia baada ya ajali" kilichotokea ni........!!!!

Mbunge Joseph Mbilinyi (SUGU), akizungumza na wanahabari mkoani Mbeya kuhusu ajali hiyo.

Gari la mbunge Joseph Mbilinyi (SUGU) baada ya kupata ajali.
Gari la polisi linalotumiwa na askari wa usalama barabarani (trafik) katika eneo la tukio Isanga (barabara ya Chunya) Mbeya.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

Kampuni ya Studio Maisha yatoa fursa kwa wasichana wenye umri kuanzia 18-22 !!!



Mtendaji Mkuu wa MAKEKE AFRIKA,  Mbunifu wa mavazi Jocktan Makeke akimwandaa mmoja wa wanamitindo wakati wa zoezi  la upigaji wa picha na kampuni ya Studio MAISHA katika mradi wa African Queen.

Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mbeya kimetoa tamko la kupinga hukumu iliyotolewa dhidi ya dereva wa Shanta Mining alie sababisha ajali kwa waandishi watatu!!

Kulia ni mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mbeya Bw. Modest Nkulu akitoa taarifa kwa waandishi wa habari hawapo pichani, kushoto ni mweka hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mbeya Bi. Esther Macha.

Jumatatu, 12 Desemba 2016

Habari njema kwa Wajasiriamali!!



Mwandaaji wa chapa ya Mkulima Market, Dkt. Vicensia Shule akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza tukio hilo. Kushoto kwake ni  Mratibu wa Vikundi vya Kilimo na Ujasiriamali katika Mkulima market, Steven Peter Mfuko.

Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye Soko la Wazi- Mkulima Market, litakalofanyika tarehe 22, 23 na 24 Desemba 2016 (Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi) katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkabala na UDASA Club huku waandaaji hao wakitoa nafasi 30 kwa wajasiriamai wadogo kushiriki kwenye tukio hilo kwa bei ya punguzo.

Jumanne, 6 Desemba 2016

Serikali inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri, kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii!!

Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii wakiwa katika picha ya pamoja wakiji selfisha (selfie) na Waziri wa Habari mh. Nape Nnauye, hivi karibuni katika mkutano  mkuu wa mwaka wa waandishi wa habari za mitandao ya kijamii (TBN) uliofanyika jijini Dar es salaam.

Mwandishi wa habari za mtandao wa kijamii wa Mbeya yetu ndg. Joseph Mwaisango, akipeana mkono na Waziri wa Habari mh. Nape Nnauye,  katika mkutano wa waandishi wa habari za mitandao ya kijamii (TBN) uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.

SERIKALI inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.

Serikali yatangaza Mradi wa Ajira ya Dharura Sekta ya Afya, jumla ya watumishi 192 wanahitajika katika Halmashauri 40!!.



TANGAZO LA KAZI
MRADI WA AJlRA YA DHARURA KATlKA SEKTA YA AFYA

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali champango wa Ajira ya dharura kwa wataalamu wa "fani za Tabibu na Wauguzi.Mpango huu utaendeshwa chini ya mradi, kwa ufadhili wa fedha za Mfuko wa CDC, Award No. 5U2GGH001062-03 kwa muda wa miaka miwili.

Rais Magufuli,asema ni marufuku kuwaondoa Wamachinga jiji Mwanza, awataka wamachinga warejee katika maeneo yao ya biashara hadi hapo watakapo tengewa maeneo rasmi!!

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Baba wa miaka 57 anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 4!!

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia bw. Severini Elius(57), mkazi wa Kijiji cha Mabogini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Binti wa miaka 20, amejichoma kisu tumboni kisa mama yake kumhoji sababu za kushika ujauzito ili hali ana mtoto mdogo!!


Polisi mkoani Ruvuma inamshikilia binti mwenye umri wa miaka 20 Eva Kapinga, mkazi wa kata ya Mateka Halmashauri ya Manispaa ya Songea, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake, Catherine Kapinga mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu (1.5), kisha nae kujichoma kisu tumboni kwa lengo la kutaka kujiua.

Jumatatu, 5 Desemba 2016

Mwanafunzi darasa la 5, aliekuwa amehamishwa shule kutoka kijijini kwenda mjini, amejinyonga.!!,


Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kizota Manispaa ya Dodoma, Yassin Abdallah (13) amejinyonga kwa kutumia shuka la bafuni baada ya kupata matokeo mabaya ya mitihani yake ya mwisho wa mwaka.

Ndugu wa 3 na wengine 2, wamefariki usiku wa leo, baada ya kilabu cha pombe za kienyeji walichokuwa wakikitumia kugongwa na lori!!.

Nyumba iliyokuwa ikitumika kama kilabu ikiwa imebomoka baada ya kugongwa na lori 
lori la mizingo lenye namba za usajili T801 ACD,lililo sababisha ajali na vifo vya watu 5 

Ajali iliyo sababisha vifo vya watu 5, imetokea usiku wa leo mkoani Iringa baada ya lori la mizingo lenye namba za usajili T801 ACD lililokuwa likielekea mkoani Mbeya kuacha njia na kugonga kilabu cha pombe za kienyeji.

Waziri Mpina aeleza kitakacho ifanya Serikali ya awamu ya 5, isiyumbe wala kuyumbishwa!!


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa Kinziga, Salasala Jijini Dar es Salaam.

NAIBU  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema Serikali ya awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za Mungu katika kuwatumikia wananchi wake na si vinginevyo.

Jumapili, 27 Novemba 2016

HIFADHI YA TAIFA UDZUNGWA YACHANGIA MADATI 1062 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 128.

Kushoto ni Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha, akizungumza na wanahabari hivi karibuni.

Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha,  akiwaelezea jambo waandishi wa habari (hawapo pichani)


Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha mesema kuwa Hifadhi ya Taifa Udzungwa imechangia jumla ya madawati 1062 yenye thamani ya sh. 128 milioni katika shule  za msingi 18 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu Wilayani Kilombelo Mkoani Morogoro.

Akizungumza na wanahabari wanawake kutoka katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania ambao walitembelea hifadhi hiyo ya Udzungwa, Simon amesema hifadhi hiyo imechangia kiasi hicho cha madawati kupitia mradi wa Ujirani Mwema  na kwamba  madawati hayo yametolewa kwa awamu tatu.

Akafafanua zaidi kuwa awamu ya kwanza Tanapa ilichangia madawati 414 yenye thamani y ash. 56 milioni madawati hayo yalipelekwa katika shule za msingi 17 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu, awamu ya pili madawati 278 yenye thamani ya sh.26 milioni ambayo tayari yamesha kabidhiwa katika shule za msingi 18 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kitatu , na awamu ya tatu ni madawati 370 yenye thamani y ash. 46 milioni ambayo yatakabidhiwa hivi karibuni baada ya kukamilisha taratibu za kukabidhi kwa shule  18 ambazo zipo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu Wilayani Kilombelo mkoani Morogoro.
  
Navasha akaongeza kuwa  TANAPA ilianza mchakato wa kuchangia madawati katika vijijini vinavyopakana na hifadhi ya Udzungwa tangu mwaka 2013 ambapo alibainisha kuwa miongoni mwa vigezo ambavyo vinatumika katika kuchagua ni kijiji ama shule gani zipewe madawati  au miradi mingine yenye lengo ya kuwasaidia wananchi waishio katika vijiji vinavyo pakana na hifadhi  hiyo ni pamoja na kuangalia vijiji ambayo vimekuwa vikitii sheria za uhifadhi bila shuluti kama kushiriki kutoa taarifa za ujangili, kuto kata miti, kuto choma moto,  kutofanya shuhuli za uwindaji ndani ya hifadhi nk.

Hata hivyo Naivasha amesema kuwa ipo miradi mingi ya ujirani mwema,  miongoni mwa miradi hiyo ni pamoaja na ujenzi wa vyumba vya madarasa,ufugaji wa kuku hususani kwa wakina mama, ufugaji nyuki, ufugaji ngombe na mbuzi, ambapo miradi ya ufugaji imeanzishwa katika maeneo ambayo wakazi wake hususani wanaume walikuwa wakijihusisha zaidi na shughuli za uwindaji ndani ya hifadhi.

Naivasha amefafanua kuwa dhumuni la kuanzisha miradi ya ujirani mwema ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa ni kuondoa migogoro baina ya wakazi waishio maeneo ya karibu na hifadhi na Tanapa, kuimarisha kudhibiti wa vitendo vya ujangili,  kwani kupitia miradi hiyo Tanapa inapata nafasi ya kutoa elimu kwa wananchi kila inapobidi kufanya hivyo.

Akizungumzia changamoto ambayo Tanapa inakumbana  nayo katika kutekeleza miradi hiyo ya ujirani mwema, ‘’changamoto kubwa tunayo kabiliana nayo ni ugumu wa wananchi kuchangia ile asilimia ndogo wanayopaswa kuchangia, mnajua kwa kawaida Tanapa tunachangia 70% na wananchi nao wanatakiwa kuchangia 30% lakini wanakuwa wagumu kutoa” alisema Naivasha.

Kuhusu sababu zinazopelekea wananchi hao kuwa wagumu kuchangia hata kwa kiasi kidogo wanachopaswa kuchangia Naivasha amesema ni matumaini makubwa ya wananchi. “unajua wananchi wengi wanaamini kuwa Tanapa ina hela nyingi sanaa pia hela hizo zinatolewa na serikali, hivyo kuna tunapata changamoto kubwa sana tunapoenda kukabidhi miradi hiyo ukiwaambia wanatakiwa kuchangia wanaona kama wewe ulieenda kukabidhi  mbaya hivyo wananchi wanamatumaini makubwa kupita kiasi hiyo ndiyo changamoto” alisema Naivasha.


Alimaliza kwa kutoa wito kwa wananchi waishio maeneo jirani na hifadhi kutambua kuwa jukumu la kuzilinda hifadhi nila kila mwananchi pia akawataka washiriki vema katika kuisaidia Tanapa kupambana na vitendo vya kijangili ambavyo vinashamiri kwa kasi.