Jumamosi, 26 Machi 2016

Hongera sana mbunge viti maalum Vicky Kamata kwa kufunga ndoa,

Dk Servacius Likwelile akiwa na mkewe 
Vicky Kamata baada ya kufunga ndoa

Mbunge wa Viti Maalamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vicky Kamata amefunga ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile.

Dk Likwelile amefunga ndoa hiyo baada ya mkewe wa awali kufariki dunia Mei mwaka 2014.

Kwa hatua hiyo, Dk Likwelile amemfuta machozi mbunge huyo kijana baada ya ndoa yake ya awali aliyotarajia kuifunga na Charles Pai kukwama dakika za mwisho wakati wa maandalizi yote ya msingi kukamilika.
                                          
Inadaiwa kuwa mbunge huyo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya , alifunga ndoa hiyo Septemba mwaka jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Wawili hao baada ya kufunga ndoa, hawakuwa na sherehe kubwa bali walikuwa na pati iliyofanyika nyumbani kwa Dk Likwelile na kuwashirikisha baadhi ya wana ndugu na marafiki wa pande zote mbili.

Kamata alikiri kufunga ndoa hiyo, lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi.

“ni kweli nimefunga ndoa, ninachojua ni kwamba Dokta Likwelile ni mume wangu halali, namshukuru Mungu kwa hilo,”

Mei 24 mwaka 2014, Vick Kamata alikwama kufunga ndoa na Charles Pai baada ya kubainika kuwapo kwa kasoro kwenye nyaraka za mwanaume.

Hali hiyo ilisababisha mbunge kuugua ghafla kutokana na mshituko alioupata na kulazimika kulazwa katika Hospitali ya Tabata Genaral iliyopo Segerea. Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilikuwa zimesambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge. Ambazo inaelezwa zaidi y ash. Milioni 90 za mchango zilichangwa na wadau mbali mbali ili kufanikisha ndoa ya Vicky Kamata

Kamata ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha “ Wanawake na Maendeleo” na pia ni mtetezi wa haki za wanawake.

Mwaka 2014 ulikua ni kipindi cha machungu na maumivu makali kwa Vicky Kamata kwakua ndoa yake iliyeyuka ghafla na kumsababishia hali yake kiafya kua taabani, wakati kwa upande wa  Dk Servacius Likwelile ambaye sasa ni mume halali wa Vicky Kamata yeye alifiwa na mkewe kipenzi hali iliyopelekea majonzi,

Baada ya yote kutokea hatimae kwa wakati mmoja wote wamejikuta wakiwa katika furaha na faraja kubwa baada  wawili hao kufunga ndoa na kuwa bibi na bwana

mwaka 2014 Vicky Kamata akiwa amelazwa
 katika Hospitali ya Tabata Genaral 
iliyopo Segerea Jijini Dar es salaam baada ya
 kupata mshituko kutokana na ndoa yake
 kuyeyuka ghafla.
hawa ni baadhi ya wapambe walio takiwa kuwepo
 katika harusi ya Vicky hapo wakiendelea
 kumfariji mgongwa huku wakiwa katika 
vazi la sare ambalo lilitakiwa kuvaliwa ukumbini 
katika harusi ya Vicky, na haikujulikana 
kwanini waliamua kuvaa baada ya ndoa
 kubuma au ndio ilikua kutoa nuksi?  
                                             
Kila lakheri Vicky Kamata katika ndoa yako hongera kwa kushinda maumivu ya kutendwa, 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni