Alhamisi, 28 Januari 2016

shindano la tuzo ya (ubobezi wa fikra za afrika) The African MisterMind kufanyika Mbeya mwezi wa pili


dr. Joshua Lawrence mkurugenzi wa mipango na mikakati wa taasisi ya Dream success enterprises (njozi ya mafanikio)

kijana akiwa amevaa T-shirt ambazo washiriki watazivaa katika shindano hilo

Dada akiwa amevaa T-shirt ambazo washiriki watazivaa 



Log 
Moja ya kipeperushi cha The African Mastermind chenye maelekezo ya namna ya kuweza kushiriki katika tuzo hiyo

shindano la tuzo ya ubobezi wa fikra za afrika (The MasterMind African Award)  linatarajiwa kufanyika Mbeya tarehe 28/2/ 2016 katika ukumbi wa Mkapa Hall uliopo Sokomatola, ambapo zoezi hilo litaendelea katika mikoa mingine kama, Mwanza, Arusha, Mtwara na mikoa mingine na hatimae fainali za shindano hilo kufanyika katika Jiji la dar es salaam,

Hayo yamesemwa na dr. Joshua Lawrence ambae ni mkurugenzi wa mipango na mikakati wa taasisi hiyo alipokua akizungumza na Blog hii hapo jana,

Dr. Lawrence amesema awali uzinduzi wa tuzo hiyo ulipaswa kufanyika dar es salaam lakini ukaahirishwa baada ya maoni ya wadau mbali mbali kushauri kuwa kwa kua fainali itafanyikia dar es salaam basi ni vyema uzinduzi ukaanzia katika mikoa ambayo itashiriki katika tuzo hizo ambapo kwa mujibu wa mapendekezo ya wadau mchakato wa kuwapata washiriki wa tuzo hiyo utaanzia jiji Mbeya hapo tarehe 28.2.2016 sanjari na kuwapata washiriki,

Dr. Lawrence amesema tuzo hiyo itatolewa kwa watu ambao watakua wameonyesha mawazo chanya ya namna ya kuisaidia Afrika iweze kupiga hatua za maendeleo,

Na kwamba vigezo vya kushiriki katika  tuzo hii dr.Lawrence alisema  mtu yeyote  awe ni mwanamke au wanaume wenye umri kuanzia miaka kumi na sita (16) na kuendelea anaruhusiwa kushiriki bila kujali kiwango cha elimu na kwamba kinacho angaliwa ni fikra.

Akifafanua zaidi kuhusu namna unavyoweza kushiriki alisema washiriki wanatakiwa kujaza form maalumu ili waweze kupewa namba ya ushiri na kisha kisha watatakiwa kuwasilisha live hotuba walio iandaa wakielezea “kwanini afrika pamoja na kua na rasilimali za kila namna bado watu wake wangali masikini na tutafanyaje ili tutoke hapa”?

Aidha alisema kwa wale ambao wapo mbali lakini wangependa kushiriki katika shindano hili pia wanaruhusiwa kushiriki na kwamba wao watalazimika kuandaa video clip ya hotuba isiyozidi dakika 10 kisha kuiwasilisha wakielezea kwanini afrika pamoja na kua na rasilimali za kila namna bado watu wake wangali masikini na tutafanyaje ili tutoke hapa? Kisha ataituma clip hiyo katika whatsApp namba 0744- 683-511,

Lawremce amesema washiriki wote wana ruhusiwa kutumia lugha ya moja wapo kati ya hizi Kifaransa, Kiingereza au Kiswahili,
Na kwamba kuna zaidi ya milioni mia tano (500m) zimetengwa kwa ajili ya shindano hilo

washindi watakabidhiwa tuzo ya kombe ambalo litakua ni ukumbusho wa ushiriki wake huku wale watakao fikia  kumi bora video clip zao zitaingizwa kwenye mfumo wa dokumentari (documentary) kisha zitasambazwa katika nchi za afrika,

Dr. Joshua alimaliza kwa kuelezea uzoefu wa taasisi hiyo ya Dream success enterprises (njozi ya mafanikio) katika kuandaa tuzo mbali mbali nchini ambapo alitaja baadhi ya tuzo ambazo zimewahi tolewa na taasisi hiyo kua ni pamoja na tuzo ya SHUJAA KATI YETU ambapo mtunukiwa wa kwanza wa tuzo hiyo alikua ni mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali bw. Ludovick Utouh ambae kwa sasa amestaafu,

tuzo nyingine ya SHUJAA KATI YETU ilitolewa mwaka jana 2015 kwa watu watatu ambao ni Vicky Mtetema aliekua mtangazaji wa BBC alipewa tuzo kutokana na ubunifu na ujasiri wake wa kupambana na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)  wanapewa haki yao na kulindwa,

Saed Kubenea alipewa tuzo ya umahili wa kuandika habari na kutumia kalamu katika kuelimisha umma na mtu mwingine aliye pewa tuzo hiyo Mh. David Kafulila ambae alipewa tuzo kutokana na ujarisi wake katika suala zima la kuhakikisha kwamba watanzania wananufaika na rasilimali zilizomo hasa katika scandle ya ESCROW
Kwa maoni, swali na ushauri kuhusu tuzo hii piga namba

 0744- 683-511 (namba hii ni maalumu kwa ajili ya shindano hili na imesajiliwa kwa jina la MasterMind)

Maoni 3 :

  1. mbona hiyo fomu ya usajili wa kushiriki ilo shindano siioni au ndo muda umeisha?

    JibuFuta
  2. kama ipo naomba nitumiwe kwa gmail acount hii alexkatowo@gmail.com

    ahsanteee!!!!

    JibuFuta
    Majibu
    1. Habari, Alex Katowo napenda kukufahamisha kuwa shindano hili lipo, lakini pia kwa maoni na ushauri kuhusu shindano hilo tafadhari piga simu namba 0744 683 511, namba hii imesajiliwa kwa jina la The MasterMind na ni maalumu kwa ajili ya shindano hili, ahasante kwa kuitembelea blog ya tuonane, tuendelee kushirikiana

      Futa