Ijumaa, 8 Julai 2016

Waziri Jenista Muhagama akonga nyoyo za wakazi wa kijiji cha Mbaka Wilayani Rungwe waliokua wakivuka dalaja kwa kutumia kamba kwa miaka kadhaa, Azam Tv yamwagiwa sifa!!

Muonekano wa dalaja lililopewa jina la Kivuko cha Jenista Muhagama
Baada ya kituo cha Azam Tv kuripoti habari ya wakazi wa kitongoji cha Kibundugulu kulazimika kuvuka daraja kwa kutumia kamba hatimae mwezi mmoja baadae daraja hilo limejengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 58

Mnano mei 19 mwaka huu Azam ilitembelea daraja hilo na kujionea hali halisi ambapo serikali ilichukua hatua za makusudi na kuanza kulijenga,

Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho walikua wakilazimika kuvuka mtoni pasi kujali usalama wao Azam Tv ilishuhudia baadhi ya watoto wakilazimika kuvua nguo ili kuweka kupita ndani ya maji huku wazee, vijana na baadhi ya watoto wakilazimika kupita katika kamba jambo ambalo lilikua ni hatari.

Kufuatia taarifa iliyoripotiwa na kituo cha Azamu Tv kuhusu adha wanayopata wakazi wa kitongoji cha Kibundugulu katika kijiji cha Mbaka Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya mwezi mmoja baadae daraja hilo lilijengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 58

Mkazi wa eneo hilo aliejitambulisha kwa jina la Subila Kaleke alisema Ujenzi wa daraja hilo ulianza baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Muhagama  kuzulu katika eneo hilo

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla amesema uzinduzi wa dalaja hilo umeacha historia katika kijiji cha Mbaka ambapo katika kufurahia uzinduzi huo wananchi pamoja na viongozi walipata chakula cha pamoja.

Kwa upande wake kaimu Mhandisi Wilaya ya Rungwe bwana Lugano Mwambingu alikipongeza kituo cha Azam Tv kwa kuibua changamoto ya dalaja hilo.


Mwandishi wa Azam Tv-Kakuru Musim  ambae ndie alie ibua habari ya dalaja hilo -  akipita katika dalaja baada ya uzinduzi.

Mkazi wa kijiji cha Kibundugulu katika kijiji cha Mbaka Wilayani Rungwe mkoani Mbeya (picha na Kakuru).
Wakazi wa kijiji cha Kibundugulu katika kijiji cha Mbaka wakipita kwa shida katika dalaja hilo kabla ya kujengwa
mkazi wa kijiji cha Kibundugulu katika kijiji cha Mbaka wakipita kwa shida katika dalaja hilo kabla ya kujengwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni