Jumapili, 6 Machi 2016

Wanafunzi wa Chuo cha Mtega Nursing kilichopo Chimala Mkoani Mbeya wapewa elimu ya matumizi sahihi ya Internet,


wanafunzi wa chuo cha Mtega Nursing Chimala wakisikiliza kwa umakini



Baadhi ya wanafunzi wakifurahi baada ya kupata somo la matumizi sahihi ya Internet na Mitandao ya kijamii
Wanafunzi wa chuo cha Mtega Nursing kilichopo Chimala Mkoani Mbeya, wapewa elimu ya matumizi sahihi ya Internet na Mitandao ya kijamii

Wanafunzi wa chuo cha Nursing Mtega kilichopo chimala wapewa somo la matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na blog hii ofisini kwake Mkurugenzi wa chuo hicho bw. Francis Mtega amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo ya kumtafuta mtaalamu wa masuala ya kijamii ili aweze kutoa elimu kwa wanachuo wake kama njia moja wapo ya kujenga maadili mazuri kwa wanafunzi wanapokua wakitumia mitandao au Internet,

“wanafunzi wengi wahawatumii vizuri Internet wengi hupoteza mda kwa kuangalia picha za ngono na vitu vingine visivyo na maadili, mtandao ni mzuri kama wanafunzi watajua matumizi yake kwa kutafuta vitu muhimu kama vitabu mbali mbali ambavyo vimewekwa katika mtandao.” alisema Mtega.

Baadhi ya wanafunzi walio hudhulia wakati somo hilo likitolewa walisema walikua hawajuwi kwamba unaweza kupa mambo ya msingi na sahihi katika mtandao wa Internet, kwa sasa kupitia elimu hiyo wamejifunza kwamba wanaweza kua na makundi ya kujadiliana mambo ya kuhusu kozi wanazo somea,

“kwa sasa hata mimi nita elimisha wenzangu kuhusu matumizi sahihi ya mtandao kwa wanafunzi, tunaushukuru uongozi wa chuo kwa kutuletea wataalamu na kutufundisha elimu hii. Alisema Agness Mazengo.

Kwaupande wake Ephraim ambaye ndie alikua muwezeshaji katika somo hilo la matumizi sahihi ya mtandao wa Internet alisema wanafunzi wengi hupoteza muda mwingi  katika mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Facebook, Twitter, Instergram, Viber na mitandao mingine ya kijamii kwa kuandika matusi au kuangaila mambo ya ngono.

Ndugu Ephraim pia alisema ni jukumu la kila kuhakikisha  kwamba vijana wanatumia mitandao vizuri, hii mitandao imerahisiha mawasiliano, sasa unaweza uka nakili au download mambo muhimu, kwa sasa watu wanasoma vyuo mbali mbali ulaya kupitia mtandao wa Internet,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni