Ijumaa, 11 Machi 2016

Tangazo: Nafasi za masomo kwa kozi mbalimbali za afya, Muda wa mwisho wa kuomba kujiunga ni tarehe 31 Marchi, 2016

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

 MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO MARCHI 2016/2017.









Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto  kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wanatangaza nafasi za masomo kwa kozi mbalimbali za afya zinazotolewa na vyuo vilivyosajiliwa na NACTE na kutambuliwa na wizara.
Kufuatia tangazo hili watu wote wanaopenda kujiunga na kozi hii, watume maombi yao ili wajiunge na kozi hizi ifikapo mwezi April 2016.

1.        Kozi zinazotangazwa ni:  

A.      Kozi za ngazi ya Stashahada:
(i)         Maabara (Diploma in Medical Laboratory Sciences)
(ii)        Utabibu (Diploma in Clinical Medicine)
(iii)       Uuguzi  (Diploma in Nursing)

B.      Kozi za ngazi ya Astashahada (Cheti)
(i)         Maabara (Certificate in Medical Laboratory Sciences)
(ii)        Utabibu  (Technician Certificate in Clinical Medicine)
(iii)       Ufamasia (Certificate in Pharmaceutical Sciences)
(iv)       Uuguzi  (Certificate  in Nursing)

C.      Kozi za ngazi ya Astashahada ya Awali (Basic Technician Certificate).
(i)     Dispensers (Basic Technician Certificate in Pharmaceutical Sciences)
(ii)   Community Health Worker -CHW (Basic Technician Certificate in Community Health)

2.       Muda wa Mafunzo:   
(i)     Miaka mitatu (3)kwa kozi za Stashahada (Ordinary Diploma)
(ii)    Miaka miwili (2) kwa kozi za astashahada (Technician Certificate)
(iii)   Mwaka mmoja (1) kwa astashahada ya awali (Basic Technician Certificate)


3.       Sifa za Muombaji Watarajali (Pre-service):
(i)    Awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’,  kwa masomo ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia, Hisabati na Kingereza kwa kozi za Stashahada (Ordinary Diploma).

(ii)   Awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia, Fizikia, Hisabati na Kiingereza kwa kozi za  Astashahada (Technician Certificate).

(iii)  Awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ‘D’, kwa masomo manne (4), likiwemo somo la biolojia (Biology) kwa kozi za Astashahada ya awali (Basic Technician Certificate)

4.  Utaratibu wa kutuma maombi:
Maombi yatafanyika kwa  njia ya mtandao kupitia mfumo wa udahiri wa pamoja (Central Admission System-CAS) unaoendeshwa na kusimamiwa na NACTE.Aidha mfumo huu unapatikana kupitia Tovuti: www.nacte.go.tz  au  www.cas.go.tz 

5.       Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
a) Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) litakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote         watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya Baraza na pia kupitia utaratibu mwingine wowote utakaodhihirika kurahisisha mawasiliano na utoaji taarifa.  
b)Taarifa hizo zitatumwa pia vyuoni kwa ajili ya ufatiliaji na urahisishaji wa mawasiliano.

6.  Muda wa mwisho wa kuomba kujiunga ni tarehe 31 Marchi, 2016.

7. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 18 April, 2016.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
S.L.P. 9083,

6 Barabara ya samola machel,11417. Dar es Salaam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni