Ijumaa, 12 Februari 2016

Alie husika moja kwa moja na kutungua helikopta (chopa) ahukumiwa kifungo cha miaka 20, huku akisubiri kesi nyingine mbili, na ndie mdogo kuliko washtakiwa wote,

rubani Rogers Gower enzi za uhai wake

Helikopta (chopa) iliyotunguliwa



 Mahakama ya Wilaya ya Bariadi imewahukumu watu wanne, mmoja kifungo cha miaka 20 jela na watatu miaka 15 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya hatia ya kukutwa na silaha ambazo zilitumika kutungua helikopta kwenye Pori la Akiba Maswa wilayani Meatu na kusababisha kifo cha rubani wake Rogers Gower raia wa Uingereza,
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Simiyu Mary Mrio alisema anawapa adhabu hiyo washtakiwa hao baada ya kukiri kosa la kukutwa na silaha hiyo kinyume cha sheria na hivyo kutoisumbua mahakama.
Katika hukumu hiyo, Njile Gunga ambaye anadaiwa kutungua ndege hiyo Januari 29 atatumikia kifungo cha miaka 20, huku akisubiri kesi nyingine mbili ya mauaji ya rubani  na uhujumu uchumi ambazo zitatajwa Mahakama ya Mkoa wa Simiyu. 
Waliohukumiwa kifungo hicho mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya, Mary Mliyo, ni Mange Buluma (47), Shija Mjika (38), Dotto Pangali (41) na Njile Gunga (28), ambao wamehukumiwa kutumika kifungo cha miaka 15 jela kila mmoja kwa kosa la pili kati ya makosa 11 waliyoshtakiwa.

Hakimu Mliyo alisema kesi hiyo iliyokuwa na washtakiwa tisa, wengine walikana makosa yao yakiwamo ya kukutwa na silaha na risasi ambao ni, Mange Buluma, Moses Masasi na Mwigulu Kanga, hivyo kurudishwa mahabusu na kesi yao itaendelea Februari 24, mwaka huu.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Yamiko Mlekano alitaja makosa hayo kuwa ni kumiliki na kukutwa na silaha kinyume cha sheria.
Shtaka la tatu ni kukamatwa na risasi tano za bunduki aina ya rifle, shtaka ambalo Pangali na Gunga walikiri.
Katika shtaka la nne linalowakabili washtakiwa wote wanne, Wakili Mlekano alidai ni umiliki risasi kinyume cha sheria, ambazo walikamatwa nazo Februari 8 na bunduki aina ya Rifle 303.
Washtakiwa hao waliomba kupunguziwa adhabu kwa kile walidai ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama hayo, lakini Mlekano aliomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Hakimu Mrio alisema kwa kosa la kwanza, pili na nne mahakama inawahukumu kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja, kosa la tatu miaka mitano au kulipa faini ya Sh10 milioni.    
Ikumbukwe kuwa washtakiwa hao walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kwa mara ya kwanza Februari 10, mwaka huu kwa kosa la kutungua helikopta 'chopa' na kusababisha kifo cha rubani wake, katika pori la akiba la Maswa wilayani Meatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni