Jumamosi, 13 Februari 2016

Wa Tanzania waishio nchini Malawi wafunguka sawa sawa kuhusu siku 100 za utawala wa Dr. John Pombe Magufuli na utumbuaji Majipu na Vijipu


muonekano wa jiji la Blantyre nchini Malawi

muonekano wa Jiji la Blantyre - Malawi 

Wa Tanzania waishio nchini Malawi wamezungumzia siku mia moja za Dr. John Pombe Magufuli akiwa madarakani, wakizungumza kwa nyakati tofauti na ripota wa DW ambae pia ni muandishi wa  habari wa kituo cha redio Galaxy kilichopo nchini Malawi bw. Ephraim  Mkali Banda,

Wananchi hao ambao ni wa fanyabiashara katika jiji la Blantyre Nchini Malawi wamesema wanafurahishwa na utendaji kazi wa  Rais John Pombe Magufuli,

Faraja Kyando anaeishi Nchini Malawi kwa ajili ya shughuli za biashara  amesema anamshukuru mungu kwa kutupa kiongozi bora ambae alikua ni hitaji wa watanzania kwa muda mrefu na hatimae amepatikana huku akisema kuwa siku mia moja za utawala ya Dr. John Pombe Magufuli umeleta matumaini makubwa kwa watanzania huku imani kubwa ikiwa ni kuzaliwa kwa Tanzania mpya,

Pia Faraja alibainisha sababu zinazopelekea watanzania kua na imani kubwa katika utawala wa rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli kua ni namna rais alivyosimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato, alivyoweza kutimiza baadhi ya ahadi alizozitoa katika kipindi cha kampeni kama elimu bure, kutatuliwa kwa migogoro ya ardhi huku akitolea mfano kurejeshwa kwa mashamba makubwa ambayo yamekua chini ya wawekezaji  kwa muda mrefu jambo ambalo limekua likipelekea migogoro ya mara kwa mara na ufuatiliaji wa muenendo wa  utendaji kazi katika mahakama nchini, na kuongeza kua mahakama ni miongoni mwa chombo ambacho kimekua kikilalamikiwa na kungung’unikiwa na wananchi wa hali ya chini kutokana na kuto tenda haki mf ucheleweshaji wa kesi, kuto tenda haki wakati wa hukumu nk,

Aidha faraja alieleza namna anavyolichukulia suala la Rais anavowatimua kazi (kutumbua majipu) baadhi ya watendaji ambao wanabainika kuto timiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kanuni za sheria za kazi, ambapo Faraja alisema anaunga mkono utaratibu huo, na kufafanua kuwa rais yupo sahihi kuwatimua watendaji hao kwani watendaji hao wamekua wakikata tawi walio likalia bila kujua mwisho wa siku tawi likianguka na wao wataanguka aki maanisha kuwa kiongozi aliepewa dhamana anaposhindwa kutimiza wajibu wake aliopewa kwa makusudi au kwa maslahi binafsi ni sawa na kukata tawi alilokalia hivyo watendaji hao wanapo anguka hawatakiwi kumlaum rais,

Mtanzania mwingine anaeishi Malawi kwa shughuli za kibiashara katika mji wa SunSide jijini Blantyre Nchini Malawi amesema tathmini yake juu ya siku mia moja za utawala wa Dr.John Pombe Magufuli ni kua anaamini kuwa mungu amesikia kilio na maombi ya watanzania na kuwapa walichokua wakikihitaji na hivo imani yake ni kwamba Tanzania ya miaka 40 iliyopita inarejea tena kutokana na utendaji wa JPM, kwani ni kiongozi ambae anauchungu na nchi yake pia wananchi wa hali ya chini wanaokula mlo mmoja

Akizungumzia timua timua ya rais dhidi  ya watendaji wabovu  alimaarufu kama (kutumbua majipu) hali ambayo imekua gumzo nchini na hata katika nchi nyingine jirani na kusababisha hisia tofauti huku wengine wakimtafsiri Rais kua ni udikteka na wengine wakisifia kua ni uongozi bora uliotukuka ,

mfanya biasha huyo amesema hashangazwi na suala hilo kwa kua hata katika ngazi ya familia watoto wanazeza kumwita baba dikteta kutokana na utaratibu anaotaka kwenda nao huku akitolea mfano kuwa hadhani kama kuna baba ambae anaweza akakubali mtoto afanye mambo nje ya matakwa yake hivyo hata hao wanaomsemea vibaya na kubeza kasi ya Rais Magufuli ni dhahiri kua nao ni sehemu ya majipu na vijipu kwa kua Rais huwatimua watendaji wabovu na wazembe.

Rais wa awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli


Blog hii inatoa shukrani nyingi kwa Ephraim Mkali Banda repoter wa Dw, kwa kufanya mahojiano hayo na Watanzania waishio Malawi kwani hii huonyesha ni jinsi gani sasa watanzania wanajivunia utanzania wao na wanafurahia kuwa watanzania kwani tumeshuhudia siku za nyuma baadhi ya watanzania hususani vijana walio kata tama wakijutia kua watanzania na kulazimika kutumia misemo mbali mbali inayowakilisha hisia zao kama “ni bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuwa binadamu Tanzania” 

Maoni 2 :

  1. Hari hiyo safi sana huo ndio uhusiano nzuri wa wana habari

    JibuFuta
    Majibu
    1. ahsante kwa maoni yako Hawa Ahmed, ahsante kwa kuitembelea blog hii ya tuonaneblog, tuendelee kushirikiana

      Futa