Jumanne, 7 Juni 2016

Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kufanya mapenzi na binti yake wa miaka 9


Mkazi wa Moshi njiapanda ya Himo daniel Mshana 42 amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya ngono na binti yake wa kumzaa.

Suala hilo liligunduliwa na walimu katika shule aliyokua akisoma mtoto huyo mwenye umri wa miaka tisa baada kumuona siyo mchangamfu na ufaulu wake darasani kuanza kuporomoka.

kwamujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, baada ya mtoto huyo kuonesha hali hiyo mwalimu wa darasa alimuhoji ndipo alipoeleza mkasa mzima na suala hilo kufikishwa polisi.

inaelezwa kua mshtakiwa ambae ni baba mzazi wa mtoto huyo alikua akiishi na mtoto wake huyo baada ya kutengana na mkewe ambaye aliondoka na watoto wawili na kumwacha  binti huyo na baba yake.

Hukumu hiyo ilitolewa ijumaa iliyopita na hakimu mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro Anthony Ngowi aliyesema ketendo alichokifanya mshtakiwa ni kibaya kisichopaswa kufumbiwa macho na jamii.

Wakili wa serikali Kanda ya Moshi Ignas Mwinuka alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa tarehe tofauti kati ya oktoba na Novemba 23, 2015
aidha alisema kua kosa alilotenda mzazi huyo ni kinyume cha kifungu cha 158 cha kanuni za adhabu, kifungu hicho kinasema mwanamume yeyote anayefanya mapenzi na mjukuu , mtoto wake, dada au mama yake anatenda kosa la kufanya mapenzi na maharimu.

akitoa hukumu hiyo hakimu ngowi alisema ushahidi wa mashahidi sita akiwamo mtoto mwenyewe daktari na walimu umeithibitishia mahakama kuwa mshana alitenda kosa hilo.

Kabla ya hukumu hiyo wakili Mwinuka aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa vile vitendo vya aina hiyo vinaanza kuongezeka nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni