Jumatatu, 6 Juni 2016

Yanga yasajili wawili kwa mpigo


Yanga wamefanikiwa kumsajili golikipa wa Prisons Benno Kakolanya na Vicent Andrew kutoka Mtibwa Sugar kama beki wa pembeni

Yanga wamefanikiwa kumsajili golikipa wa Prisons Kakolanya na Vicent Andrew kutoka Mtibwa Sugar kama beki wa pembeni

Wafalme wa soka ya Tanzania, Yanga SC wamefanikiwa kumsainisha kipa wa Prisons ya Mbeya na Taifa Stars, Benno Kakolanya mkataba wa miaka miwili.

Kakolanya amesema kwamba amesaini Yanga baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka mitatu Prisons ya Mbeya.
“Nimesaini miaka miwili kujiunga na Yanga, baada ya kumaliza Mkataba wangu Prisons,”amesema kakolanya ambaye ni kipa wa tatu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.


Kakolanya alionyesha uwezo mkubwa msimu huu akicheza mechi 19 za ligi kuu na kufungwa mabao manane tu huku akiisaidia Prisons kumaliza katika nafasi ya nne mbele ya Mtibwa iliyomaliza ikiwa nafasi ya tano.
Kakolanya sasa anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne

alie anguka chini ni Vicent Andrew kutoka Mtibwa Sugar akiwajibika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni