Jumapili, 10 Julai 2016

Zaidi ya watu 300 nchini wamefanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa Vikope (Trakoma)

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt.Mwele Malecela  akimfariji  bi.Neyo Marias mkazi wa kijiji cha mtimmoja mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa vikope(trakoma). Tanzania zaidi ya wagonjwa mia tatu wamekwishafanyiwa upasuaji huo.

Watu zaidi ya mia tatu nchini wamefanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa vikope(Trakoma) kutokana na serikali kuweka mikakati ya kuyatokomeza na kuyaondoa kabisa.

Hayo yamesemwa leo na mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu dkt. Mwele Malecela wilayani mnduli wakati wa zoezi la uhamasishaji wa umezaji dawa za kuzuia trakoma na upasuaji wa ugonjwa huo.

Dkt. Malecela amesema zoezi hili ambalo ni endelevu kwa wilaya zilizoathirika na ugonjwa huu inasaidia kumaliza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

 Aidha wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanakunywa dawa, kufanyiwa upasuaji pamoja ya kuwa safi wao pamoja na mazingira wanayoishi.
Mmoja wa shuhuda toka kitongoji cha Nongwe Juu bw. Kesoi Ng'utoki (kushoto) ambaye alifanyiwa upasuaji wa vikope kwenye zoezi kama hili mwaka jana, kulia ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Nongwe Juu bw. Klamian Ng'utoki.



Watoto wakipatiwa kingatiba ya ugonjwa wa trakoma aina ya Zithromax na watoa huduma wa afya kwenye moja ya boma lililop kwenye kijihi cha mtimmoja. Mkoa wa Arusha wilaya zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo ni monduli,Ngorongoro na Longido.

Baadhi ya wakazi wa kijijo hicho wakisubiri kupatiwa kingatiba  ya ugonjwa wa trakoma (Picha zote na Catherine sungura - wizara ya  afya).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni