Jumamosi, 26 Machi 2016

Hongera sana mbunge viti maalum Vicky Kamata kwa kufunga ndoa,

Dk Servacius Likwelile akiwa na mkewe 
Vicky Kamata baada ya kufunga ndoa

Mbunge wa Viti Maalamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vicky Kamata amefunga ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile.

Dk Likwelile amefunga ndoa hiyo baada ya mkewe wa awali kufariki dunia Mei mwaka 2014.

Kwa hatua hiyo, Dk Likwelile amemfuta machozi mbunge huyo kijana baada ya ndoa yake ya awali aliyotarajia kuifunga na Charles Pai kukwama dakika za mwisho wakati wa maandalizi yote ya msingi kukamilika.
                                          
Inadaiwa kuwa mbunge huyo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya , alifunga ndoa hiyo Septemba mwaka jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Wawili hao baada ya kufunga ndoa, hawakuwa na sherehe kubwa bali walikuwa na pati iliyofanyika nyumbani kwa Dk Likwelile na kuwashirikisha baadhi ya wana ndugu na marafiki wa pande zote mbili.

Kamata alikiri kufunga ndoa hiyo, lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi.

“ni kweli nimefunga ndoa, ninachojua ni kwamba Dokta Likwelile ni mume wangu halali, namshukuru Mungu kwa hilo,”

Mei 24 mwaka 2014, Vick Kamata alikwama kufunga ndoa na Charles Pai baada ya kubainika kuwapo kwa kasoro kwenye nyaraka za mwanaume.

Hali hiyo ilisababisha mbunge kuugua ghafla kutokana na mshituko alioupata na kulazimika kulazwa katika Hospitali ya Tabata Genaral iliyopo Segerea. Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilikuwa zimesambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge. Ambazo inaelezwa zaidi y ash. Milioni 90 za mchango zilichangwa na wadau mbali mbali ili kufanikisha ndoa ya Vicky Kamata

Kamata ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha “ Wanawake na Maendeleo” na pia ni mtetezi wa haki za wanawake.

Mwaka 2014 ulikua ni kipindi cha machungu na maumivu makali kwa Vicky Kamata kwakua ndoa yake iliyeyuka ghafla na kumsababishia hali yake kiafya kua taabani, wakati kwa upande wa  Dk Servacius Likwelile ambaye sasa ni mume halali wa Vicky Kamata yeye alifiwa na mkewe kipenzi hali iliyopelekea majonzi,

Baada ya yote kutokea hatimae kwa wakati mmoja wote wamejikuta wakiwa katika furaha na faraja kubwa baada  wawili hao kufunga ndoa na kuwa bibi na bwana

mwaka 2014 Vicky Kamata akiwa amelazwa
 katika Hospitali ya Tabata Genaral 
iliyopo Segerea Jijini Dar es salaam baada ya
 kupata mshituko kutokana na ndoa yake
 kuyeyuka ghafla.
hawa ni baadhi ya wapambe walio takiwa kuwepo
 katika harusi ya Vicky hapo wakiendelea
 kumfariji mgongwa huku wakiwa katika 
vazi la sare ambalo lilitakiwa kuvaliwa ukumbini 
katika harusi ya Vicky, na haikujulikana 
kwanini waliamua kuvaa baada ya ndoa
 kubuma au ndio ilikua kutoa nuksi?  
                                             
Kila lakheri Vicky Kamata katika ndoa yako hongera kwa kushinda maumivu ya kutendwa, 

Ijumaa, 25 Machi 2016

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee


Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na wazee wa mkoa wa Dare s Salaam walipokutana katika kikao ofisini kwake (Katikati) ni Mwenyekiti wa baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali na kulia ni katibu wa wazee hao  Mohamed Mtulia.
Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali akizungumza katika kikao cha wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto).
Katibu wa  wazee wa Dar es Salaam Mohamed Mtulia (Kulia) akizungumza wakati wa kikao  Mhe. Ummy mwalimu (kushoto) na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu(Kulia) akionesha kitabu cha sera ya wazee ambayo inatarajiwa kuandikiwa mswaada wa kuwa sheria na kupelekwa Bungeni kushoto ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.

Kaimu kamishna Ustawi wa Jamii Rabikira Mushi akizungumza katika kikao cha wazee wa Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Dar es Salaam Bi. Mary Chipungahelo(maarufu kama mama Chips) akichangia mada katika kikao kati ya baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
 Serikali imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.

Mpango huo umetolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam alipokutana nao mapema wiki hii ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. amesema wazee wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.

“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bunge mwezi Septemba ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza masuala yahusuyo wazee” Alisema Mhe.Ummy.

Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.

Aidha Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.

Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli  kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee nchini.

MWISHO

Mkuu wa mkoa Dar Es Salaam Poul Makonda afanya ziara kwa viongozi wa dini awaomba wampe baraka zao

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es SalaamKadinali Pengo akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ofisini kwake makao makuu ya Kanisa Katoliki, Forodhani
Kadinali Pengo akimuombea Paul Makonda
Picha ya pamoja bada ya maombi na maongezi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata baraka na busara zao 

Makonda ameanza ziara hiyo rasmi jana ambapo alimtembelea  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo 

Aidha siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya kisasa.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, leo anatarajia kukutana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum

Jumatano, 23 Machi 2016

ukweli kuhusu watu watatu walio uawa kwa kunyongwa kisha miili yao kuchomwa moto huko wilayani Kyela mkoani Mbeya, maswali yasiyo na majibu yaendelea kutawala katika hisia za wengi!


Hiki ndio chumba kilichokua na miili yote mitatu ya marehemu  hao

haya ndio maelezo yao waliyo yaandika katika daftari la wageni katika gesti waliyo kua wamefikia
Polisi wakitoa miili ya marehemu (siku ya jumapili)

Gari lililobeba miili ya marehemu hao kutoka hospitali ya Kyela kuipeleka Mbeya mjini
Kaka wa marehemu Zauda Omari na Baraka Chaula ambao ni ndugu (kaka na dada  
Mwenye kikoi cha kimaasai ndie mume wa marehemu Zauda Omar 
Kaka wa marehemu Zauda Omari na Baraka Chaula ambao ni ndugu (kaka na dada
akiwa katika majonzi makubwa
Maiti za watu watatu waliouawa kikatili baada ya kunyongwa na miili yao kuchomwa moto ndani ya chumba kimoja zimetambuliwa, wamo ndugu wa familia moja.

Wakati taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa juzi na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, ikiwataja marehemu hao kuwa ni Mariam Hassan, Abbas yasini na Tatizo Adamu wote wakazi wa Songea, Mkoani Ruvuma.

Hata hivyo, baada ya ndugu hao wa marehemu kuwatambua, wametaja majina halisi ya marehemu hao na kusema kuwa si wakazi wa Songea, bali wote ni wakazi wa Jijini Mbeya katika maeneo ya Ilomba na Mbarali, na kwamba si wafanyabiashara kama walivyokua wamejiandikisha wao katika daftari la wageni katika gesti waliokua wamefikia.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Riziki Chaula, aliyejitambulisha kuwa ni kaka wa marehemu wawili, aliwataja marehemu hao kuwa ni Zauda Omar (34) , Mkazi wa Ilomba, Jijini Mbeya na Baraka Chaula (28) Mkazi wa kijiji cha Utulo kata ya Mapogolo, Wilayani Mbarali ambao ni ndugu.

Alimtaja marehemu watatu kuwa ni Rodgers Simwaka, Mkazi wa Ilomba, Jijini Mbeya na kwamba ni jirani wa marehemu Zauda na amekuwa akijihusisha na shughuli za kusajili laini za simu katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya.

Aliongeza kuwa, mbali na marehemu Zauda kuwa ni mdogo wake waliochangia baba, lakini pia alikuwa ni mke wa mtu na hadi mauti inamfika walikuwa wakiishi kwa amani na mumewe aliyemtaja kwa jina la Abdalah Malifyuma.

“Vifo hivi vimetuacha kwenye mkanganyiko mkubwa sana….kwani Zauda na Baraka ni dada na kaka mtu na huyo mwingine ni jirani yao, sasa iweje watoke Mbeya hadi Kyela na kukutwa wakiwa wamenyongwa ndani ya chumba kimoja” alihoji Riziki.

Aidha, Riziki aliongeza kuwa, siku moja kabla ya tukio marehemu Zaudi alikuwa amewasiliana na majirani zake, pamoja na mumewe na kuwaaga kuwa alikuwa na safari ya kwenda na kurudi Wilayani Rungwe.

Licha ya majirani wa marehemu Zauda kusimulia jinsi walivomfahamu marehemu na kuishi naye, lakini mume wa marehemu huyo alikataa kuzungumza chochote juu ya tukio hilo la mauaji, huku muda wote akionekana kulia kwa hisia kali.

Mmoja wa majirani wa marehemu Zauda, Said Nkenja alisema siku moja kabla ya tukio marehemu alimtaarifu  kuwa angesafiri kwenda kwenye shughuli zake Mjini Tukuyu, Wilayani Rungwe na kwamba taarifa za kuuawa kwake zimewashitua na kuzua hofu kubwa.

Kwa upande wake, rafiki wa karibu na marehemu Rodgers, aliyejitambulisha kwa jina la Sebastian Aman, alisema siku mbili kabla ya tukio la kuuawa kikatili kwa rafiki yake ambaye walikuwa wakifanya kazi ya kuuza laini za simu, alimuaga kuwa atakua  na safari kikazi ya siku tatu ya kwenda Wilayani Chunya.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Kyela, Dk.Frencis Mhagama, alithibitisha miili ya marehemu hao kutambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao baada ya kukaa hospitalini hapo kwa siku 3

Maiti hizo zilikutwa kwenye chumba kimoja zikiwa zimefungwa mifuko ya rambo usoni huku zikiwaka moto.


Hata hivyo bado chanzo cha mauaji hayo ya kikatili hakija julikana haswa ukizingatia wawili ni ndugu mmoja kati yao ni jirani, swali je? walikua na agenda gani huko kyela ukizingatia alikuwepo kaka na dada akiwemo jirani, kwanini wote walidanganya kuhusu eneo wanalotarajia kwenda pindi walipo waaga majirani kabla ya safari? ni nani alietekeleza unyama huo je ndie aliewaita huko?

Jumanne, 22 Machi 2016

Baada ya matokeo ya Meya wa jiji la Dar kutangazwa Freeman Mbowe azungumzia kauli ya Rais "Acha demokrasia ichukue nafasi"

Meya wa Jiji Isaya Mwita Charles 
Meya wa Jiji Isaya Mwita Charles anayeungwa mkono na Ukawa ndiye Meya wa Jiji la Dar baada ya kupata kura 84 dhidi ya Yenga Omari (CCM) aliyepata kura 67.

Akizungumza na waandishi mara baada ya kutangazwa mshindi Mwita amesema kua nchi yetu itapiga hatua kubwa haswa jiji la Dar Es Salaam  endapo viongozi na wananchi watashirikiana na  kuweka pembeni itikati za vyama.

Mwita amesema kua kwa kua Rais John Pombe Magufuli ametabainisha kua anataka kuwasaidia watanzania hivo kwa kushirikiana kwa pamoja na kuweka itikati pembeni nchi itapiga hatua.   

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Freeman Mbowe akizungumza mara baada ya matokeo kutangazwa na Chadema kuibuka na ushindi amesema ushindi wao haujatokana na kauli la Rais ambayo aliitoa jana Ikulu

Rais magufuli alisema acha demodrasia ichukue nafasi yake” akimaanisha kua demokrasia itumike kumpata Meya Jiji hilo, kauli hiyo imeibua hisia kua huenda imechangia kuipa ushindi Chadema

Mbowe amesema kua ushindi wao umetokana na kura za wananchi kwani  Rais amekuwepo kwa kipindi miezi mitano huku akishuhudia ufedhuli ambao umekua ukitendeka katika mchakato wa kumpata Meya,
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Freeman Mbowe 

Chadema kimepata ushindi katika uchaguzi wa umeya wa Dar es salaam baada ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa mara kadhaa. Hii ni mara ya kwanza kwa CCM kushindwa kutwaa kiti cha meya.

Aidha mara baada ya matokeo kutangazwa kuliibuka nderemo na vifijo kutoka wananchi kufurahia ushindi huo wa Bw. Mwita 

Rais John Pombe Magufuli, atuma salamu za rambirambi kwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa Njombe

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
                                       
                                          OFISI YA RAIS,
                                                  IKULU,
                                        BARABARA YA BARACK OBAMA,          
                                                                              11400 DAR ES SALAAM,   
                                                                                                  TANZANIA,
                                                                                                    

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi:255-22-2113425








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi, kufuatia kifo cha ghafla cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, Kilichotokea jana jioni tarehe 21 Machi, 2016.
Bi. Sara Dumba aliugua ghafla kuanzia jana mchana na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Njombe (Kibena), ambako wakati akipatiwa matibabu alifariki dunia majira ya saa moja za jioni.
Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushitushwa na kifo cha ghafla cha Bi. Sara Dumba, ambaye amesema alimfahamu kwa uchapakazi wake, uaminifu na uadilifu katika utumishi wa umma na katika uongozi.
"Nimeshitushwa sana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, kwa mara nyingine Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikuwa bado unahitajika" amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amebainisha kuwa Marehemu Sara dumba atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuhimiza maendeleo ya wananchi, hususani katika kilimo na ufugaji, kuhimiza nidhamu ya utumishi serikalini na kuwatetea wananchi wa hali ya chini wakati wote wa majukumu yake ya ukuu wa wilaya.
Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mkubwa, katika kipindi hiki kigumu na pia amewataka wote kuwa na subira na uvumilivu.
Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
22 Machi, 2016

MABASI YAENDAYO KASI KUFANYIWA MAJARIBIO WIKI HII JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mabasi yaendayo kasi (DART) yataanza kufanyiwa majaribio ndani wiki moja kuanzia sasa ili madereva waanze kuzoea njia na taa za kuongozea magari.

“mabasi kati ya 30 – 50 yatapita kwenye njia zote za mradi huo. Zoezi hilo litafanyika ili watumiaji wengine wakiwemo waendesha daladala, bodaboda na watembea kwa miguu waweze kutambua kuwa njia ya mabasi yaendayo kasi si ya kwao, hivyo waanze kuzoea,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi.



 alizungumzia mradi wa mabasi yaendayo kasi  wakati akijibu maombi ya mfanyabiashara mmoja, Bw. Sharifu Ramadhani ambaye alisema wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya usafiri kwa vile mabasi mengi yanaishia Mnazi Mmoja. “Mabasi yanaishia Mnazi Mmoja na huku ni mbali kwa hiyo tunalazimika kutembea kwa miguu kwa sababu kukodi taxi ni gharama kubwa,” alisema.

Akifafanua kuhusu hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi huo, Majaliwa alisema: “Hivi sasa wanakamilisha ufungaji wa mitambo ya kukatia tiketi ambapo abiria atakuwa na kadi kama za benki ambayo anaijaza fedha halafu anapita kwenye mashine, kiasi cha nauli kinakatwa halafu anaingia kwenye basi, hakutakuwa na muda wa kukata tiketi.”

Alisema tatizo la usafiri kwa wafanyabiasha wa feri litakwisha hivi karibuni baada ya mabasi hayo kuanza.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MACHI 22, 2016.

Jumatatu, 21 Machi 2016

Tanzia, Mkuu wa Wilaya Njombe Sarah Dumba afariki dunia ghafla

Sarah Dumba enzi za uhai wake, hapo akiongea na wananchi wa kijiji cha Welela Kata ya Mtwango Wilayani Njombe 

Taarifa tulizozipata hivi punde zinasema mkuu wa wilaya ya Njombe Mh. Sarah Dumba amefariki dunia ghafla jioni ya leo, kwa mujibu wa chanzo cha habari Bi, Sarah alikua ofisini hadi mida ya saa tisa jioni ambapo alianza kulalamika kua anajisikia vibaya, akapelekwa katika Hospital ya wilaya Kibena ambapo muda mufupi alifariki dunia, blog hii inatoa pole kwa familia, wana Njombe na wadau wa maendeleo nchini






Mwanahabari Salma Said wa Dw, aelezea mateso aliyoyapata baada ya kutekwa


Mwanahabari wa Dw, Salma Said Nitaeleza kwa ufupi sana kwa kweli ni unyama na uhuni mkubwa niliofanyiwa ilikuja gari pale airport wakati nikisubiri gari yangu na kuniingiza kwa nguvu katika gari na kunipeleka sehemu wakanifungia na kunipiga sana kisha wanaondoka wanarudi tena wananipiga tena kwa hivyo machungu juu ya machungu maumivu makali sana hawakuwa wanachagua mateke vibao uso ulivimba sana waliponiona pumzi zishanibana nahangaika ndio wakafunga mlango wakatoka nje wakaniacha mpaka asubuhi wakaja tena wakawa wananipiga tu na kusema maneno yao ya vitisho kumbe kosa langu kubwa ni kuandika habari za Mazombi wakinambia najifanya mwandishi na mtetezi wa haki za wanyonge huku wakinipiga na kuniahidi hawataniachia mpaka Dk Shein.

Na jana ndio wakanirejesha kule kule waliponichukua karibu na kituo cha Taxi cha airport wakiwa wamenifunika uso na kunitupa tu saa 11.30 Alfajiri nilipojifunua ndio nikajikuta nipo hapo nikajiburura hadi kituoni nikaongea na mama mmoja hapo anisaidia akanambia kaa chini mwangu akawa ananiliwaza ndio baadae nikachukua taxi kwenda Aga khan hospitali daktari wangu hakuwepo ikabidi niende Regence Hospitali tokea asubuhi hadi hiyo saa 10 alipokuja Onesmo kunichukua na kwenda polisi kuweka taarifa na kuhojiwa hadi saa 4 usiku. Simu yangu muda mwingi nilikuwa nayo mwenyewe na ndio siku ya mwanzo nilipoongea walipokuja wakanipiga sana sana na muda mwingine simu wakaizima ila hawakuichukua na hawajachukua chochote kwa kuwa walisema shida yao nisiripoti uchaguzi tu


Rais mstaafu wa Malawi Joyce Banda adaiwa kuishi kwa kujificha, akwepa mkono wa sheria, mumewe anena kuhusiana na kujificha kwa mkewe

habari na Ephraim Mkali.
Joyce Banda
Ken Msonda
                                Khumbo Kachali                                       
Kiwewe na uchu wa madaraka umeingia ndani ya Chama tawala cha zamani nchini Malawi cha People (PP),

chama hicho kinasemekana kusimamisha kazi aliyekua kua Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Ken Msonda kwa madai kua anashirikiana na alieye kua makamu wa rais katika utawara wa Joyce Banda bw. Khumbo Kachali, kuleta mpasuko ndani ya chama hicho.

Msonda amefanya kazi ya ukatibu Mkuu wa chama hicho kwa miaka miwili, kwa sasa chama hicho kimemteua Joseph Chikwamba kua katibu tawara mpya,

Uteuzi huo umethibitishwa kwa vyombo vya habari na katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Ibrahim Matola na kusema ''ni jambo la kawaida chama kufanya mabadiliko''

Akizungumza na muandishi wa habari hii Msonda amesema kwamba kwamba yeye haja ng'olewa na uongozi wa chama bali alijiudhulu mweyewe kwenye kiti hicho cha ukatibu mkuu tawara

''Nashanga kwamba chama kinasema kwamba kimenisimanisha kazi wakati mimi nimeomba kupumzika tena kwa barua, leo hii wanatangaza kwamba wamenisimamisha, nashanga kabisa'' alisema Msonda.

Pia Msonda alikanusha taarifa za kwamba yeye amekua anafanya mikutano ya siri na Kachali ya kupanga mbinu za kumuondoa Joyce Banda kwenye chama hicho.

Miezi kadha iliyopita wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa chama hicho walinukuliwa wakisema Joyce Banda anatakiwa kurudi nyumbani Malawi ambapo kwa sasa yuko mafichoni tangu alipo anguka katika uchaguzi uliofanyika Mei 2014.

Tangu Joyce Banda aondoke kwenda mafichoni mambo mengi yamekua yaki jitokeza ndani ya chama chake hicho ambapo aliyekua mugombea mwenza katika uchaguzi wa mwaka 2014 Sositen Gwengwe alikihama chama hicho na ku jiunga na chama cha Malawi Congress,

Hadi sasa haijulikani lini Joyce Banda atarejea nyumbani kujenga na kuimarisha chama chake.

Mhadhiri wa maswala ya siasa katika chuo kikuu cha Chancellor College Professor Bone Dulani amesema kuna umuhimu Joyce Banda kurudi nyumbani kujenga chama chake lakini pia amemtaka Banda kumteua kiongozi moja atakae simamia chama hicho hadi pale atakaporejea nyumbani.

Kwa tarifa zilizo patikana kuhusu Joyce Banda zisema anashindwa kurejea Malawi kutoka alikojificha kwa kuhofia  kufunguliwa mashitaka ya ubadhilifu wa fedha uliotokea katika utawara wake.

Hivi karibuni vyombo vya habari nchini Malawi vilimnukuu mume wa rais mstafu Joyce Banda Jaji Mkuu mstafu Richard Banda akisema usalama wa mke wake ni mdogo endapo mke wake atarudi Malawi.

Katiba ya nchi ya Malawi haijaweka kinga kwa rais kuto shitakiwa baada ya kuachia madaraka, rais wa kwanza kushitakiwa nchini Malawi alikua Bakili Muluzi na mali zake zingine zili taifishwa kutokana na kuhujumu uchumi kulikojitokeza katika kipindi chake cha utawala mwaka 1994 hadi 2003