Alhamisi, 18 Mei 2017

"Polisi jijini Arusha wakana kuwasomba waandishi na karandiga, wadai waliwapa Lift"

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Claud Gwandu

Katika hali ya sintofahamu mapema leo jijini  Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia kusanyiko la watu walioongozwa na mstahiki Meya wa jijji la Arusha Kalisti Lazaro Bukhay,  kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba katika  ajali uliyopoteza uhai wa dereva, walimu na Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.




Tukio hilo kwenda kutoa rambirambi pia lilihudhuriwa na Madiwani,  viongozi mbalimbali wa dini  pamoja na waandishi wa habari lilikuwa likiendelea kufanyika katika eneo la shule hiyo ambapo ghafla polisi  walifika na kuwaweka chini ya ulinzi.



Inaelezwa kuwa baada ya polisi hao kuwaweka chini ya ulinzi waliondoka nao wote wakiwemo Waandishi wa habari wapatao kumi, lakini katika hali ya kushangaza baada ya kufika kituo cha polisi cha kati polisi hao waliwaachia huru waandishi kwa madai kuwa hawana shughuli nao bali waliwapa lift tu kutoka kwenye eneo la tukio hadi kituoni hapo.




Hata hivyo katika mkutano uliofanyika dakika chache baada ya waandishi hao kuachiwa huru, Polisi walidai alie amuru polisi kuwashikilia wote waliokuwa wamekusanyika  kwa lengo la kutoa rambirambi hakujua kama kulikuwa na waandishi na kwamba  hawakuwa na kosa lolote na ndio maana waliachiwa muda mfupi baada ya kufika kituoni.


Kufuatia tukio hilo,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) imelaani tukio hilo.




Katika hatua nyingine meya wa jiji la Arusha, madiwani, walimu, mmiliki wa shule ya lucky Vincent, viongozi wa dini waachiwa huru kwa dhamana kwa sharti la kufika kituoni hapo kila watakapoitajika kufanya hivyo.


Shule ya lucky Vincent lipata pigo mnamo may 6.2017 majira ya saa 4 asubuhi kufuatia  ajali iliyotokea katika eneo la Rhotia wilaya ya Karatu na kusababisha  vifo zaidi ya 30 vikiwahusisha  wanafunzi, walimu na dereva, ajali hiyo ilitokea  wakati wakielekea kushiriki mtihani wa kirafiki wa moko na wenzao wa shule ya msingi Tumanini Junior 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni