Muonekano wa dalaja lililopewa jina la Kivuko cha Jenista Muhagama |
Baada ya kituo cha Azam Tv kuripoti habari ya wakazi wa kitongoji
cha Kibundugulu kulazimika kuvuka daraja kwa kutumia kamba hatimae mwezi mmoja
baadae daraja hilo limejengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi
milioni 58
Mnano mei 19 mwaka huu Azam ilitembelea daraja hilo na kujionea
hali halisi ambapo serikali ilichukua hatua za makusudi na kuanza kulijenga,
Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho walikua wakilazimika kuvuka
mtoni pasi kujali usalama wao Azam Tv ilishuhudia baadhi ya watoto wakilazimika
kuvua nguo ili kuweka kupita ndani ya maji huku wazee, vijana na baadhi ya
watoto wakilazimika kupita katika kamba jambo ambalo lilikua ni hatari.
Kufuatia taarifa iliyoripotiwa na kituo cha Azamu Tv kuhusu adha
wanayopata wakazi wa kitongoji cha Kibundugulu katika kijiji cha Mbaka Wilayani
Rungwe Mkoani Mbeya mwezi mmoja baadae daraja hilo lilijengwa na serikali kwa
gharama ya zaidi ya shilingi milioni 58
Mkazi wa eneo hilo aliejitambulisha kwa jina la Subila Kaleke
alisema Ujenzi wa daraja hilo ulianza baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Muhagama kuzulu katika eneo hilo
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla amesema uzinduzi wa
dalaja hilo umeacha historia katika kijiji cha Mbaka ambapo katika kufurahia
uzinduzi huo wananchi pamoja na viongozi walipata chakula cha pamoja.
Kwa upande wake kaimu
Mhandisi Wilaya ya Rungwe bwana Lugano Mwambingu alikipongeza kituo cha Azam Tv
kwa kuibua changamoto ya dalaja hilo.
Mwandishi wa Azam Tv-Kakuru Musim ambae ndie alie ibua habari ya dalaja hilo - akipita katika dalaja baada ya uzinduzi. |
mkazi wa kijiji cha Kibundugulu katika kijiji cha Mbaka wakipita kwa shida katika dalaja hilo kabla ya kujengwa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni