Maziwa ya mtindi hunywewa na
hata kuwa mboga na chakula kwa watu wengi, lakini sasa kwa wanawake ni muhimu
sana kunywa kwa lengo la kukabiliana na ugonjwa wa fangasi.
Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) umeeleza kuwa asilimia 70 hadi 90 ya wanawake nchini wanashambuliwa na
aina mbalimbali za fangasi.
Wameeleza kuwa fangasi hizo zinatokana na sababu mbalimbali ambazo
wanawake wanakumbana nazo katika maisha ya kila siku, ikiwemo ujauzito,
matumizi ya kondomu kwa muda mrefu, kuchangia tendo la ndoa na mwanamume zaidi
ya mmoja, nguo, maji, matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari na mazingira.
Utafiti huo umebaini sababu zinazochangia wanawake wengi
kushambuliwa na vijidudu vya fangasi ikiwemo wanawake wenyewe kushindwa
kujihifadhi vizuri. Aliongeza kuwa katika utafiti huo, walibaini pia kuwa
wanawake wamekuwa wakishambuliwa na aina zaidi ya nne za fangasi.
Sababu nyingine alisema ni kutodhibiti matumizi ya sukari, ambapo
fangasi huelemea kuta za seli na kuzalisha vimeng’ enya ambavyo hufyonza
virutubisho na kuingia katika damu.
Fangasi baadaye huanza kujipenyeza kwenye damu, mapafu, moyo na
hatimaye kushambulia figo ambapo huleta magonjwa nyemelezi na njia pekee ya
kutibu ni kutumia mtindi mara kwa mara na kutumia dawa ambazo pia zinahitaji
ushauri kwa daktari.
Utafiti huu ni muhimu kwa wanawake wote kuchukua hatua katika
kupambana na fangasi ambao wakianza huwezi kujua kama wana maradhi kiasi hicho,
lakini kila mmoja ahakikishe anatumia mtindi ambao ni chakula na dawa.
FAIDA NYINGINE YA MAZIWA MTINDI :
Mtindi
unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho
vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.
Vikitajwa kwa
uchache virutubisho hivyo, imethibitika kuwa mtindi ni chanzo kizuri cha ‘Calcium’,
‘Phosphorus’, ‘Riboflavin (vitamin B2), ‘Iodine’, ‘vitamin B12’, ‘Pantothenic
acid (vitamin B5) ‘Zinc’, ‘Potassium’ na ‘Molybdenum’. Mbali ya virutubisho
hivyo, ndani ya mtindi kuna ‘bakteria hai’ ambao ni muhimu kiafya katika mwili.
HUREFUSHA MAISHA:
Utafiti
unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee,
uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa mbalimbali umeonesha kuongezeka na
kufanya mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi.
Katika utafiti
mmoja, walichaguliwa wazee 162 ambao walipewa utaratibu wa kunywa mtindi na
maziwa zaidi ya mara 3 kwa wiki na kufuatiliwa maendeleo yao kwa muda wa miaka
mitano. Baadaye utafiti huo ulionesha kuwa idadi ya vifo vya wazee hao
ilipungua kwa asilimia 38 ukilinganisha na kundi la wazee wasiotumia au
waliotumia mtindi kiasi kidogo sana.
KINGA KWA KINA
MAMA:
Aidha, mtindi
umeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza
ukeni (vaginal infections).
Katika utafiti mmoja uliohusisha wanawake wenye
magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, baada ya kutumia mtindi kiasi cha paketi
moja kila siku kwa muda wa miezi sita, maambukizi waliyokuwanayo wanawake hao
kabla yalitoweka.
KINGA YA MWILI:
Utafiti
uliofanywa kwa wanyama, wakiwemo panya na kuchapishwa kwenye jarida moja la
masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal Of Nutrition), umeonesha kuwa
unywaji wa mtindi kila siku, huamsha na kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili
kupambana na magonjwa kadhaa ya maambukizi, ikiwemo saratani ya utumbo.
MUHIMU KUZINGATIA:
Jambo muhimu la kuzingatia
ni unywaji wa mtindi halisi uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya
ng’ombe, siyo mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga. Siri kubwa
iliyomo kwenye mtindi ni ule uchachu unaotokana na ‘bakteria hai’ wanaopatikana
baada ya maziwa kuganda na kuchachuka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni