JAMHURI YA MUUNGANO YA
TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA
JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO MARCHI
2016/2017.
Katibu Mkuu Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu
ya Ufundi (NACTE) wanatangaza nafasi za masomo kwa kozi mbalimbali za afya
zinazotolewa na vyuo vilivyosajiliwa na NACTE na kutambuliwa na wizara.
Kufuatia tangazo
hili watu wote wanaopenda kujiunga na kozi hii, watume maombi yao ili wajiunge
na kozi hizi ifikapo mwezi April 2016.
1.
Kozi
zinazotangazwa ni:
A.
Kozi za ngazi ya Stashahada:
(i) Maabara (Diploma in Medical Laboratory Sciences)
(ii) Utabibu
(Diploma in Clinical Medicine)
(iii) Uuguzi (Diploma in Nursing)
B.
Kozi za ngazi ya Astashahada (Cheti)
(i) Maabara
(Certificate in Medical Laboratory Sciences)
(ii) Utabibu (Technician Certificate in Clinical Medicine)
(iii) Ufamasia (Certificate in Pharmaceutical Sciences)
(iv) Uuguzi
(Certificate in Nursing)
C.
Kozi za ngazi ya Astashahada ya Awali
(Basic Technician Certificate).
(i) Dispensers
(Basic Technician Certificate in Pharmaceutical Sciences)
(ii) Community
Health Worker -CHW (Basic Technician Certificate in Community Health)
2.
Muda wa Mafunzo:
(i) Miaka
mitatu (3)kwa kozi za Stashahada (Ordinary
Diploma)
(ii) Miaka
miwili (2) kwa kozi za astashahada (Technician
Certificate)
(iii) Mwaka
mmoja (1) kwa astashahada ya awali (Basic
Technician Certificate)
3. Sifa za Muombaji Watarajali (Pre-service):
(i) Awe
amemaliza kidato cha nne na ufaulu wake uwe wa kiwango kisichopungua alama ya
‘C’, kwa masomo ya biologia na kemia ,
na alama ‘D’ kwa somo la fizikia, Hisabati na Kingereza kwa kozi za Stashahada
(Ordinary Diploma).
(ii) Awe
amemaliza kidato cha nne na ufaulu
wake uwe wa kiwango kisichopungua alama
‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia, Fizikia, Hisabati na Kiingereza kwa kozi za Astashahada (Technician Certificate).
(iii) Awe
amemaliza kidato cha nne na ufaulu
wake uwe wa kiwango kisichopungua alama
‘D’, kwa masomo manne (4), likiwemo somo la biolojia (Biology) kwa kozi za
Astashahada ya awali (Basic Technician Certificate)
4. Utaratibu wa kutuma maombi:
Maombi yatafanyika kwa njia ya
mtandao kupitia mfumo wa udahiri wa pamoja (Central Admission System-CAS)
unaoendeshwa na kusimamiwa na NACTE.Aidha mfumo huu unapatikana kupitia Tovuti:
www.nacte.go.tz au www.cas.go.tz
5.
Utaratibu wa kutoa taarifa kwa
waliochaguliwa:
a) Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) litakuwa
na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi
mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya Baraza na pia kupitia utaratibu
mwingine wowote utakaodhihirika kurahisisha mawasiliano na utoaji taarifa.
b)Taarifa hizo zitatumwa pia vyuoni kwa ajili
ya ufatiliaji na urahisishaji wa mawasiliano.
6. Muda wa mwisho wa kuomba kujiunga ni tarehe
31 Marchi, 2016.
7. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe
18 April, 2016.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
S.L.P. 9083,
6 Barabara ya samola machel,11417. Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni