picha hii inaonesha jinsi ugonjwa wa kisonono unavyo athiri kwa wanaume |
picha hii ikionesha jinsi ugonjwa wa kisonono ulivyo athiri miguu |
Taarifa
ya tahadhari iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) hivi karibuni
imesema, kumegundulika aina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono maarufu
kama “gono” ambavyo vinahimili nguvu za dawa (Resistant to Drugs) zinazotumika
kutibu ugojwa huo.
Tahadhari
hiyo ya WHO imesema ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya watu
ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna
hatari ya kutoweza kutibika kabisa siku zijazo.
Dalili ni mgonjwa kutokwa na usaha sehemu za siri (kwa wanaume) na kwa wanawake kusikia maumivu ya chini ya tumbo. Kutokwa na vidonda kwenye ulimi au midomoni, macho kuwa na rangi nyekundu nakadhalika.
Shirika
hilo la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza
ufuatiliaji wa aina hiyo ya kisonono kutokana na ugonjwa huo kuwa na athari
nyingi kwa binadamu kama vile mgonjwa kushindwa kupata mtoto (ugumba), mcharuko
(Inflammation), wajawazito kujifungua watoto wenye ugonjwa wa macho na huweza
kusababisha vifo.
Aina hiyo mpya ya vimelea vya kisonono vinaonesha usugu dhidi ya dawa
zote za antibayotiki zinazotumika kutibu maradhi hayo ikiwemo dawa za jamii ya
(Cephalosporins) ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni