Jumatano, 6 Januari 2016

kilimo cha maboga maharagwe na matunda dili nchini



AKULIMA nchini wametakiwa kujiunga na kilimo cha mkataba cha mboga, maharage machanga, matunda, mbegu za nyanya na mazao mengine ya mkataba, ili waweze kujiimarisha kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kikundi cha Kilimo, Biashara na Ufugaji (KIBIU) Mbuguni, Jeremia Thomas Ayo alipozungumza na tuonane blog hivi karibuni katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, Manyara.

Alisema kupitia kilimo cha mkataba, wakulima 92 wa kikundi cha Kibiu wa kata ya Shambalai na Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha, kwa ufadhili wa serikali ya Marekani wamepatiwa ruzuku ya Sh milioni 195.8 za kuimarisha mradi wao.

Alisema kwa sasa wamejengewa uwezo mkubwa kwenye kilimo kwa kuzalisha mboga zinazowapa faida wakulima na kuajiri watumishi watatu wakiwemo meneja, ofisa ugani na mhasibu.


Naye Mhasibu wa shirika la Diligent Consulting Ltd, Lilian Mrema alisema shirika lao linafanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Marekani, kupitia shirika la USADF, ambapo wanasimamia kikundi hicho cha Kibiu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni