wanafunzi wa chuo cha Mtega Nursing Chimala wakisikiliza kwa umakini |
Baadhi ya wanafunzi wakifurahi baada ya kupata somo la matumizi sahihi ya Internet na Mitandao ya kijamii |
Wanafunzi wa chuo cha Mtega Nursing kilichopo Chimala Mkoani Mbeya, wapewa elimu ya matumizi sahihi ya Internet na Mitandao ya kijamii
Wanafunzi wa chuo cha Nursing Mtega kilichopo chimala wapewa
somo la matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Akizungumza na blog hii ofisini kwake Mkurugenzi wa chuo hicho
bw. Francis Mtega amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo ya kumtafuta mtaalamu
wa masuala ya kijamii ili aweze kutoa elimu kwa wanachuo wake kama njia moja wapo
ya kujenga maadili mazuri kwa wanafunzi wanapokua wakitumia mitandao au
Internet,
“wanafunzi wengi wahawatumii vizuri Internet wengi hupoteza mda
kwa kuangalia picha za ngono na vitu vingine visivyo na maadili, mtandao ni mzuri
kama wanafunzi watajua matumizi yake kwa kutafuta vitu muhimu kama vitabu mbali
mbali ambavyo vimewekwa katika mtandao.” alisema Mtega.
Baadhi ya wanafunzi walio hudhulia wakati somo hilo likitolewa
walisema walikua hawajuwi kwamba unaweza kupa mambo ya msingi na sahihi katika
mtandao wa Internet, kwa sasa kupitia elimu hiyo wamejifunza kwamba wanaweza
kua na makundi ya kujadiliana mambo ya kuhusu kozi wanazo somea,
“kwa sasa hata mimi nita elimisha wenzangu kuhusu matumizi
sahihi ya mtandao kwa wanafunzi, tunaushukuru uongozi wa chuo kwa kutuletea
wataalamu na kutufundisha elimu hii. Alisema Agness Mazengo.
Kwaupande wake Ephraim ambaye ndie alikua muwezeshaji katika
somo hilo la matumizi sahihi ya mtandao wa Internet alisema wanafunzi wengi hupoteza
muda mwingi katika mitandao ya kijamii
kama WhatsApp, Facebook, Twitter, Instergram, Viber na mitandao mingine ya
kijamii kwa kuandika matusi au kuangaila mambo ya ngono.
Ndugu Ephraim pia alisema ni
jukumu la kila kuhakikisha kwamba vijana
wanatumia mitandao vizuri, hii mitandao imerahisiha mawasiliano, sasa unaweza uka
nakili au download mambo muhimu, kwa sasa watu wanasoma vyuo mbali mbali ulaya
kupitia mtandao wa Internet,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni