Jumatano, 23 Desemba 2015

KILIMO NA HIFADHI BORA YA VITUNGUU



1. Utangulizi
Vitunguu ni zao muhimu sana hapa Tanzania. Mikoa ya Arusha, Manyara, Iringa, Mbeya,
Tanga, Singida na Kilimanjaro ni maarufu sana kwa kilimo cha vitunguu na ni zao la chakula na
biashara kwa mkulima mdogo. Uzalishaji wa vitunguu bado ni mdogo (tani nne kwa hekta) na
upotevu wa mazao baada ya kuvuna ni mkubwa (50 %– 80%) kutokana na hifadhi duni hivyo
wakulima wanahitaji utaalamu wa kilimo bora na hifadhi ya vitunguu ili kuongeza uzalishaji na
kipato.
2.0 Uzalishaji wa vitunguu
Zao la vitunguu linazalishwa kutokana na mbegu na miche inakuzwa kwenye kitalu kabla ya
kupandikizawa shamban. Miche inakuwa na kuzaa vitunguu.Vitunguu vikikomaa, vinavunwa na
kuhifadhiwa vikiwa katika hali ya kulala bwete. Katika hali hii vitunguu vinaweza kuhifadhiwa
kwa muda mrefu aitha kwa ajili ya kuzalisha mbegu msimu unaofuata au kuuza.
Wingi na ubora wa zao la vitunguu hutegemea; hali ya hewa, aina ya vitunguu, upatikanaji wa
mbegu bora, kilimo bora, uangalifu wakati wa kuvuna, usafirishaji na hifadhi bora.
2.1 Uzalishaji
Hali ya hewa na maji
Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa vitunguu.
Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya ukavu kwa kutumia umwagiliaji. Maji mengi hasa
wakati wa masika inasababisha magonjwa mengi hasa ukungu, vitunguu haviwezi kukomaa
vizuri, hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao. Jua na hewa kavu ni muhimu sana wakati
wa kukomaa na kuvuna vitunguu.
Aina za vitunguu
Aina bora za vitunguu ni pamoja na Mang’ola red, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu
bora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40-60kgs kwa hekta ikiwa kilimo bora
kitazingatiwa.Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa kuzingatia:-
mahitaji ya soko (vitunguu vyekundu hupendwa zaidi)
musimu wa kupanda
uwezo wa kuzaa mazao mengi
uwezo wa vitunguu kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Mbegu bora
Ubora wa mbegu ni muhimu sana, kwani ndiyo chanzo cha mazao bora. Mbegu bora inatoa
miche yenye afya na kuzaa mazao mengi na bora. Mbegu za vitunguu inapoteza uoto wake upesi
baada ya kuvunwa (mwaka1). Mbegu nzuri zina sifa zifuatazo:-
Uotaji zaidi ya 80%
Mbegu safi zisiyo na mchanganyhiko
Zimefungwa vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa na unjevu.
1
Hivyo mkulima anaponunua mbegu za vitunguu azingatie yafuatayo:
Chanzo cha mbegu
Tarehe ya uzalishaji
Tarehe ya kuisha muda wake
Kifungashio cha mbegu.
Inashauriwa mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja
Mbegu bora za vitunguu zinauzwa na makampuni binafsi kama: ALPHA Seed Co., Popvriend,
Rotian Seed, Kibo Seed, East African Seed Company nk. Wasambazaji wa mbegu ni pamoja na
maduka ya TFA, na maduka ya bembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali.
Jinsi ya kuandaa kitalu na kuzalisha miche
Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.
Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na
CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.
Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati
wa kusia ili miche isisongamane.
Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo
unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.
Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota (siku7-10 kutegemea hali ya hewa).
Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.
Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani (wiki 5-6)
Matatizo ya miche kitaluni ni kama yafuatayo
:
Kuonza kwa mbegu, kunyauka kwa miche kabla na baada ya kuoto. Hali hii inasababishwa na
ugonjwa wa ukungu
“Kinyausi
” .Dawa za ukungu kama Dithane M45 au Ridomil MZnk
zinatumike kuzuia (changanya dawa na povu la sabuni ili dawa ijishike kwenye majani). Pia
uangalifu uwepo wakati wa kumwagilia maji. Mwagilia maji wakati wa asubuhi au jioni. Epuka
kumwagilia maji wakati wa jua kali kwani unjevunjevu hewani unaongeza na kusabab

Maoni 1 :

  1. Mimi nataka nianze kulima vitunguu swala la 40-60kgs kwa heka ni sahihi?

    JibuFuta