Na
Ally Daud-maelezo
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. John Kijazi ameutaka
uongozi wa hospitali ya Mwananyamala kuhakikisha kuwa dawati la malalamiko kwa
wagonjwa linafanya kazi masaa 24 ili kuboresha
huduma katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa
magodoro Dkt. Kijazi amesema kuwa wagonjwa wanatakiwa kuhudumiwa kwa wakati na
kusikilizwa malalamiko yao muda wote wanapopatwa na changamoto hospitalini hapo
ili kuweza kuboresha huduma kwa watanzania.
“Nimepata malalamiko kutoka kwa wananchi ambao
walipata matatizo usiku wa kuamkia leo na hakukuwa na mtu wa kuwasikiliza
kwa wakati na kushindwa kupata huduma
bora walipokuwa na shida hivyo naagiza uongozi kuhakikisha dawati la malalamiko
kufanya kazi masaa 24 ili kuondoa kero za Wagonjwa wote”.alisema Dkt Kijazi.
Aidha Dkt. Kijazi ameushukuru uongozi wa Umoja wa
Makanisa ya Pentekoste kwa kutoa msaada wa magodoro 50 yenye
thamani ya shilingi milioni 1.631 ili kuendeleza huduma bora kwa wagonjwa wa
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Akipokea msaada huo Dkt. Kijazi alisema kuwa anawaomba viongozi wa Umoja huo
na taasisi zingineziendelee na moyo wa kuchangia kwenye shughuli za kijamii
kadriwanavyoweza ili kuifikisha Tanzania salama katika kilele cha mafanikio.
“Nawaomba Umoja wenu, taasisi na wadhamini
mbalimbali kuweza kusaidia kuinua na kukuza huduma bora za kijamii ikiwemo
mahospitalini ili kusaidia serikali kupiga hatua katika kupambana na changamoto
ya vifaa zinazoikabili hospitali ya Mwananyamala” aliongeza Dkt. Kijazi.
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Ally
Hapi amesema kuwa ana Imani na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero za
wananchi hususani katika Wilaya yake kwani ameshaona mfano wa kupokea msaada
huo na kuungwa mkono na Katibu Mkuu Dkt. John Kijazi kwa kushirikiana vizuri
kwenye shughuli hiyo.
“Nafurahi kukutana na kushirikiana kwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi katika
shughuli za kijamii hususani katika hili la kuendeleza huduma bora zitolewazo
na hospitali ya Mwananyamala ili kuifikisha mbali Tanzania mpya” alisema Bw.
Hapi.
Msaada wa magodoro 50 yenye thamani ya shilingi Milioni
1.631 yaliyotolewa na Umoja wa Makanisa ya pentekoste ili kusaidia hospitali ya Mwananyamala leo jijini
dare s salaam.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni