![]() |
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji |
Mkazi wa kijiji cha Likweso Tarafa ya Mchoteka, kilichopo Wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma bw. Ally Mchumwa, anashikiliwa na Jeshi la Polisi , kwa tuhuma za mauaji ya Shekhe wa kijiji hicho.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma kamishna
msaidizi wa Polisi ACP Zuberi Mwombeji alisema tukio hilo limetokea Mei 22, mwaka huu, baada
ya mtuhumiwa (Mchumwa), kumfumania mkewe akifanya tendo la ndoa na sheikhe huyo.
Akitoa taarifa kamanda wa polisi amesema siku ya tukio bwana Ally Mchumwa (mtuhumiwa) na Mkewe Mariam Husein pamoja na sheikhe huyo walikua pamoja shambani wakisaiana kuvuna njugu,
Wakati zoezi hilo likiendelea bwana Mchumwa aliondoa mara moja na kuwa acha mkewe na Selemani (marehemu) wakiendelea na zoezi la kuvuna njugu na mara baada kurejea alistaajabu kuto waona shambani hapo mkewe na sheikh huyo,
Wakati mtuhumiwa akiwa katika hali ya sintofahamu hiyo alisikia sauti ikitoka porini jirani na shamba lake hali iliyo mlazimu kufuatilia sauti hizo na ndipo alipo fanikiwa kuwa mkewe na sheikhe huyo wa kiwa watupu kama walivyo zaliwa hali ilipo pelekea mtuhumia kuamini kua walikua wakifanya tendo la ndoa,
Kutokana na hali hiyo, mtuhumiwa alichomoa kisu na kumchoma nacho shingoni bw. Selemani Mwarabu na kufariki papo hapo na yeye kujisalimisha kwa uongozi wa Serikali ya kijiji na baadaye kupelekwa polisi.
"Mauaji haya yametokea saa tatu asubuhi wakati marehemu ambaye amefahamika
kwa jina la Selemen Mwalabu (45), mtuhumiwa na mkewe Mariamu Husein,
wakisaidiana kuvuna njugu shambani.
"Wakati wakiendelea na kazi hiyo, mtuhumiwa alitoka kidogo na kumuacha
marehemu pamoja na mkewe wakiendelea na kazi hiyo, aliporejea hakuwakuta
shambani hivyo akashtuka," alisema.
Aliongeza kuwa, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua
mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni