Ijumaa, 18 Novemba 2016

Sifa ya ziada inayowapa raha watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadani!!

Waandishi wa habari  wanawake kutoka kutoka katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania wametembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo katika Mkoa wa Pwani, 

Waandishi hao wapo katika ziara ya siku kumi ambapo watapata nafasi ya kutembelea baadhi ya  hifadhi zilizopo nchini kama Saadani, Mikumi, Udzungwa na Ruaha.
Saadani ni hifadhi ni miongoni mwa hifadhi za taifa zilizopo nchini yenye inavivutio  vya utalii vifuatavyo  fukwe za bahari ya hindi, utalii wa kutembelea wanyama, utalii wa kutembea kwa miguu  na utalii wa boti.
Mhifadhi utalii Bi.Apaikunda Mungure kiwa ameongozana na wanahabari mara baada ya  kuwasili katika hifadhi hiyo hivi karibuni.

Akizungumza na wanahabari wanawake  waliopo kwenye ziara hiyo, mhifadhi utalii katika mbuga ya Saadani  Bi. Apaikunda Mungule, amesema Saadan ni hifadhi pekee nchini ambayo  inasehemu ya bahari ya Hindi jambo ambalo huwafanya watalii wengi kufurahia  na kuridhika na huduma waipatayo pindi wanapotembelea hifadhi hiyo sanjari na utalii mwingine kama utalii wa kupanda boti nk.

Akizungumzia kuhusu utaratibu unaotumika kukamilisha malipo kwa watalii wa kigeni na watalii wa ndani wanaokwenda, Apaikunda amesema  kwa sasa watalii wanatakiwa kwenda na kadi ambazo hutolewa na CRDB, NMB na EXIM BANK.

Hata hivyo akafafanua kuwa dhumuni la kuweka utaratibu huo wa kadi ni  kumuepushia usumbufu mtalii anaefika katika hifadhi hiyo pamoja na kukata kodi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Saadan, bw. Lomi Ole Meikasi,  amesema hifadhi ya Saadani ni moja kati ya hifadhi kumi na sita (16) zilizopo nchini Tanzania  yenye sifa ya kipekee katika afrika mashariki kwa kuwa inasehemu ya bahari ya hindi licha ya kuwa na mazingira ya kawaida kama hifadhi nyingine zilizopo nchini.

Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Saadan na mhifadhi wa Ikologia, bw. Lomi Ole Meikasi akizungumza na wana habari  ofisini kwake. 
Amesema hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1100 ni hifadhi yenye umri mdogo ambayo ilianzishwa rasmi mwaka  2005 kwa tangazo rasmi la serikali namba 281 tarehe  16/9/2005, baada ya kulipandisha hadhi lililokuwa pori la akiba la Saadani,  na kwamba hifadhi hiyo ipo katika mikoa miwili ya Tanga  na Pwani  huku ikiwa inazungukwa na wilaya nne ambapo kwa upande wa Tanga hifadhi hiyo ipo katika wilaya za Handeni na Pangani na  Pwani hifadhi hiyo ipo katika wilaya za Chalinze na Bagamoyo na hiafadhi hiyo ina jumla ya vijiji 16 kwa Tanga na Pwani.

Akizungumzia idadi ya watalii, Kaimu huyo amesema kumekuwa na ongezeko la asilimia themanini na nne (84%) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 – 2015 ambapo  idadi hiyo imeendelea kukua kutoka watalii  3758 hadi kufikia  watalii 24145.

Kuhusu mapato amesema kuwa mwaka 2005 hifadhi hiyo ilikusanya kiasi cha milioni arobaini na tisa na laki tatu tu (49,300,000/=) na hdi kufikia mwaka 2015 hifadhi hiyo imekusanya zaidi ya bilioni moja na ishirini.

Akizungumzia namna ambavyo hifadhi hiyo inashirikiana na jamii katika kudumisha amani na ulinzi baina ya hifadhi  na vijiji jirani vinavyo izunguka hifadhi hiyo  kwa lengo la kudhibiti vitendo vya ujangiri pamoja na kutatua changamoto ya migogoro baina ya wanavijiji na hifadhi hiyo  bw. Mekasi amesema  kuwa jumla ya sh. 722,830,000/= zimetumika katika miradi mbali mbali ya kijamii kama ujenzi wa nyumba vya madarasa, kuchangia madawadi katika shule za vijiji  katika mikao ya Tanga na Pwani nk.

Hifadhi ya Saadani ina jumla ya vijiji 16 ambapo kwa upande wa Mkoa wa  Tanga hifadhi hiyo inapakana na wilaya za handeni  na Pangani  ambapo Handeni ina vijiji 4 na Pangani ina vijiji 7 na kwa upande wa Mkoa wa Pwani hifadhi hiyo inapakana na wilaya za Chalinze na Bagamomo , mbapo Chalinze ina vijiji 2 na Bagamoyo ina vijiji 3.

Picha: baadhi za vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo ya Saadani



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni