Jumanne, 6 Desemba 2016

Baba wa miaka 57 anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 4!!

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia bw. Severini Elius(57), mkazi wa Kijiji cha Mabogini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Desemba 1, 2016  saa 10 jioni, katika Kijiji cha Mabogini kata ya Mabogini wilayani na kuongeza kuwa dada wa mtoto huyo ndiye alie baini tukio hilo.
Kwa mujibu wa maelezo ya dada wa mtoto huyo mwenye umri wa mika 17  (jina linahifadhiwa) ambae ni mwanafunzi na mkazi wa mabogini amesema mzee huyo alimkuta mdogo wake akiwa nyumbani kwao peke yake  ndipo akamvamia na kumvutia chumbani na kisha kuanza kumbaka kwa nguvu.

Dada huyo akisimulia zaidi anasema baada ya kurejea nyumbani alimkuta mdogo wake akiwa analia huku akilalamika kwamba ana maumivu makali sehemu zake za siri huku akiwa anamtaja mzee huyo ambapo baada ya yeye kumchunguza alibaini kuwa amebakwa ndipo akaamua  kutoa taarifa polisi.

Maoni 1 :

  1. The Best Casino for real money in the USA - Dr.CMD
    The 포항 출장샵 Best 여주 출장마사지 Casino for Real Money in the USA · 삼척 출장마사지 Ignition Casino · Tropicana 여주 출장마사지 Casino · Microgaming · BetMGM Casino 제천 출장안마 · Barstool Sportsbook

    JibuFuta