Ijumaa, 16 Desemba 2016

Kampuni ya Studio Maisha yatoa fursa kwa wasichana wenye umri kuanzia 18-22 !!!



Mtendaji Mkuu wa MAKEKE AFRIKA,  Mbunifu wa mavazi Jocktan Makeke akimwandaa mmoja wa wanamitindo wakati wa zoezi  la upigaji wa picha na kampuni ya Studio MAISHA katika mradi wa African Queen.

Kampuni ya Studio Maisha inayojihusisha na masuala ya upigaji wa Picha  imekuja na mradi wa kuinua vipaji vya vijana hasa katika masuala ya mitindo kuanzia ngazi ya Kitaifa na Kimataifa kwa vijana wa kike na kiume kufikia malengo yao ikiwemo kwenye majukwaa ya Kimataifa.


Kwa mujibu wa wamiliki wa  mradi huo kampuni ya Studio Maisha wamebainisha kuwa, kwa kushirikiana na MAKEKE AFRIKA  kampuni ya mitindo ya kiasili wataweza kushirikisha vijana mbalimbali kufikia malengo yao hayo.


Kuhusu : “THE RISE OF AFRICAN QUEEN PROJECT”.“Kuna kauli isemayo mwanamke akiwezeshwa anaweza, kama ilivo kauli hio project hii imejikita zaid kumsaidia mwanamke hasa  mwanamke kwenye ndoto ya kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 

Wazo hili lilikuja baada ya kuona wapo wanawake wengi wenye  vipaji na wana vigezo vyote vya kuwa wanamitindo bora wa hapo baadae lakini wanakosa sapoti kuhusu wapi wataanzia na watafikaje level za kimataifa katika masuala ya mitindo”  ilieleza taarifa hiyo ya waandaaji.


Mradi huo unahusu wasichana wenye  kuanzia  umri wa miaka 18 hadi 22 pekee.  Pia kwa kila  baada ya mwezi  mmoja watu wawili ambao ni  sura mpya ‘new faces’.


Kwa sasa mradi huu umeanza  na wasichana na baadae  utaendelea  na vijana wa kiume katika “THE RISE OF AFRICAN KINGS”.  Kisha kumalizia na “THE RISE OF AFFICAN KING & QUEEN” hapo watajumuisha vijana wawili kila mwezi, yaani  wa kike na wakiume.

Waandaaji wa mradi huo wanaamini itakuwa ni fursa na mlango mpya kwa vijana kwani hawata gharamia kitu chochote na huku haki ya usambazaji wa matukio yakiwa chini ya  kampuni ya waandaaji na wadau wao  mbalimbali pia vijana watapata kushiriki katika majukwaa mbaimbali ya mitindo ya kitaifa na kimataifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni