Jumatano, 4 Oktoba 2017

Wadadisi 600 wanolewa kwa ajili ya Utafiti wa Kilimo 2016/2017!!

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma


Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo.

Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo. 

Jumla ya wadadisi 600 wamepatiwa mafunzo ya siku 5 kwa ajili ya kufanya Utafiti wa
Kilimo wa mwaka 2016/17 nchi nzima kuanzia Oktoba hadi 3 Novemba, 2017 nchi nzima.

Takwimu hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina  Chuwa  mjini Dodoma wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo na kuongeza kuwa madhumuni ya mafunzo kwa wadadisi hao ni kuwajengea uwezo wa kuhoji na kujaza madodoso ya wamiliki wa mashamba (wakulima) na namna ya kutambua mahali shamba lilipo kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho GPS.

Utafiti huu wa Kilimo wa mwaka 2016/17 unafanyika chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar (OCGS) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo amesema lengo la utafiti huo ni kutoa makadirio ya kiasi cha uzalishaji wa mazao makuu, idadi ya mifugo, mazao yatokanayo na mifugo na maeneo ya kilimo katika mikoa yote ya Tanzania.

Aidha, Mashingo ametoa wito kwa wakuu wote wa kaya watakaochaguliwa kushiriki kwenye utafiti huu,  kutoa ushirikiano wa kutosha hususan taarifa sahihi kuhusu hali ya uzalishaji wa mazao, huduma zinazotolewa na Maafisa Ugani na aina ya mbegu wanazotumia na kubainisha changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.

Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni