Jumatano, 11 Oktoba 2017

Jinsi Wafugaji walivyo danganywa na kusababisha nyumba zao zaidi ya 900 kuchomwa!!!!!

Moja ya nyumba iliyopo katika eneo la Mbuzi ndani ya Hifadhi  ikiteketea kwa moto baada ya kuchomwa katika zoezi la kuwaondoa wavamizi katika Misitu ya Asili iliyopo katika Tarafa ya Kipembawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Wananchi waliokuwa wakiishi katika Hifadhi hiyo wakiendela kuokoa mali zao wakati wa zoezi la kuwaondoa.

Mmoja ya wananchi aliyejitambulisha kwa jina la mtoto wa Singinda yatima akilia kwa uchungu baada ya nyumba yake kuteketezwa kwa moto katika operation ya kuwaondoa wavamizi  wa Hifadhi za Misitu.

Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya Mh. Mkuu wa Wilaya Rehema Madusa akiendelea na zoezi la kuchoma nyumba katika operation ya kuwaondoa wavamizi wa Misitu.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh. Rehema Madusa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusiana na madai ya wananchi (wavamizi) kuchangishwa fedha ili wasiondolewe katika Hifadhi hiyo.


Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Chunya Grace William, akitolea ufafanuzi kuhusu zoezi hilo.  

Zaidi ya watu 900 wamepoteza makazi yao baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wakishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuendesha zoezi (operation) la kuwaondoa wavamizi waliokuwa wamejenga makazi na kufanya shughuli za uzalishaji ndani ya  Hifadhi ya Msitu wa Asili uliyopo katika Tarafa ya Kipembawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani  Mbeya.

Baadhi ya wananchi hao jamii ya wafugaji waliokumbwa na kadhia hiyo ya kubomolewa na kuchomewa nyumba zao kwa moto wameelezea kushangazwa zoezi hilo na wengine wakiangua kilio na kuwalalamikia baadhi ya viongozi kwa kuwahakikishia kuwa wapo salama na kuwataka kuendeleza shughuli za uzalishaji sanjali na kuendelea kuwauzia maeneo na kuwatoza fedha  kiasi cha shilingi elfu sabini (70,000) kwa kila kaya madai kuwaa fedha hizo zilikuwa zikitumika kwa ajili ya kuwashawishi viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ili wasitishe zoezi la kuwaondoa katika maeneo hayo.

Zoezi la kuwaondoa wafugaji limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh. Rehema Madusa ambae amekiri kuwepo kwa taarifa za baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu waliokuwa wakiwachangisha fedha wafugaji hao kwa njia za udanganyifu kupitia mgongo wa Serikali kuwa hadaa kuwa zoezi la kuchangisha fedha hizo lilikuwa ni utekelezaji wa agizo la Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya na kwamba dhumuni la kuchangisha fedha hizo ni kuwatuliza viongozi ili wasitishe mpango wa kuwaondoa wavamizi.

Mh. Madusa ameongeza kuwa baada yakupata taarifa hizo ofisi yake ilichukua hatua za kwenda kuchunguza madai hayo  na kwamba kufuatia tuhuma hizo Jeshi la Polisi Wilayani humo linawashikilia watu wawili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akielezea kuhusu maandalizi ya awali yaliyofanyika hadi kufikia hatua ya maamuzi ya kwenda kuteketeza kwa kuchoma moto nyumba zaidi ya 900 za wananchi jamii ya wafugaji ili kuwaondoa katika maeneo hayo Madusa amesema Serikali ili anza kwa kutoa elimu kwa wananchi hao  na kisha kutoa notisi (notice) ya miezi mitatu ya kuwataka kuondoka katika maeneo hayo lakini wafugaji hao hawakuzingatia na kutiii maagizo ya Serikali na ndipo zoezi hilo likaamriwa kufanyia.

Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Chunya Grace William amesema Tarafa ya Kipembawe kuna Misitu zaidi ya saba inayohifadhiwa yenye ukubwa wa hekta zaidi ya laki mbili  lakini misitu hiyo imevamiwa na makundi ya watu ambao wanaendesha shughuli za kiuchumi kama Kilimo, Ufugaji, Uchimbaji na kusababisha uharibifu wa mazingira na kuongeza kuwa zoezi hilo la kuwaondoa wavamizi wa misitu ni endelevu.

                                                                 MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni