Serikali imechukua hatua hiyo baada
ya kupata malalamiko mengi kwa kile
kilichokuwa kinarushwa na kituo cha televisheni cha TBC1 cha shirika hilo
linaloendeshwa kwa ruzuku kutoka serikalini.
Agizo hilo limetolewa jana na waziri wa habari,
utamaduni,sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alibainisha kuwa amepokea simu
za watu waliokuwa wanahoji juu ya kipindi hicho, hivyo kulazimika kuchukua
hatua mara moja za kutaka maelezo kutoka kwa watendaji wa shirika hilo.
Miongoni mwa progamu za burudani na masuala ya kijami, kituo
cha TBC1 kinacho kipindi cha chereko ambacho hurushwa kila jumapili kwa matukio
ambayo yamerekodiwa, lakini hali ilikua tofauti juzi usiku baada ya sherehe za
harusi hiyo kurushwa moja kwa moja.
Kwa urefu wa muda uliotumika kurusha sherehe hizo,
watazamaji wengi walishikwa na butwaa hivyo kuzua mijadala kwenye midandao ya
kijamii wakihoji inawezekanaje kwa TBC1 kutoa muda mrefu kwa mtu mmoja kwa
ajili ya shughuli yake binafsi,
‘’Mtu hawezi kuitumia televisheni ya Taifa kwa matakwa yake,
hii ni mali ya umma, kama kila mwenye pesa atakua na uwezo wa kulipia muda wa
matangazo si muda wote tutakua tunawaona watu wenye hela tu badala ya vipindi
muhimu?’’
Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TBC1 , Clement Mshana alisema kwa kifupi
kuwa kipindi hicho ni sehemu ya vipindi vya kituo hicho cha televisheni.
“kile ni kipindi cha chereko ambacho tunacho kwenye program zetu,”
alisema mshana.
Alipoulizwa ilikuwaje ratiba ya kipindi hicho ikabadiliswa
kutoka Jumapili mpaka Jumamosi, alisema; “ Kile ni kipindi cha wikiendi na kama
mtu sherehe yake inafanyika siku hiyo, inakuwa haina shida yoyote.”
TBC ni shirika linalomilikiwa na serikali likiwa na
televisheni na redio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni