Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Bruno Kimaryo, kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza ujumbe katika mtandao wa kijamii wa kuyapongeza majambazi yaliyovamia Kituo cha Polisi cha Stakishari na kuua polisi. Aidha, mshtakiwa huyo ametakiwa ama kulipa faini ya Sh. 600,000 kwa kosa hilo.
Katika
tukio la Stakishari lililotokea Julai 12, mwaka huu, majambazi yalivamia kituo
hicho na kuua polisi wanne na raia watatu pamoja na kupora bunduki 20 aina ya
Sub Machine Gun (SMG).
Hukumu
hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Waliarwande Lema, baada ya kupitia
ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka. Alisema
vielelezo vitano na utetezi wa mshtakiwa vinaonyesha kuwa Bruno alifurahia
kitendo kilichofanywa na majambazi hao na alitamani kila kituo cha polisi
kivamiwe.
Mshtakiwa
huyo katika ujumbe wake huo alitumia viunganishi vya maneno yasiyokuwa ya
kibinadamu ya auawe, avamiwe na kuwa utetezi wake unaungana na maelezo ya onyo
aliyoyatoa polisi hayaonyeshi kusikitishwa wala kuhurumia polisi na raia walio
walio poteza maisha bila hatia.
Hakimu
Lema alisema kama mshtakiwa angekuwa anapeleka ujumbe kwa polisi wachukue
tahadhari, angeupeleka katika mamlaka husika, lakini kutokana na lugha
aliyoitumia, mahakama hiyo inamtia hatiani.
Hata
hivyo, mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa adhabu ya kifungo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni