dr. Joshua Lawrence mkurugenzi wa mipango na mikakati wa taasisi ya Dream success enterprises (njozi ya mafanikio) |
kijana akiwa amevaa T-shirt ambazo washiriki watazivaa katika shindano hilo |
Dada akiwa amevaa T-shirt ambazo washiriki watazivaa |
Log |
Moja ya kipeperushi cha The African Mastermind chenye maelekezo ya namna ya kuweza kushiriki katika tuzo hiyo |
Hayo
yamesemwa na dr. Joshua Lawrence ambae ni mkurugenzi wa mipango na mikakati wa
taasisi hiyo alipokua akizungumza na Blog hii hapo jana,
Dr.
Lawrence amesema awali uzinduzi wa tuzo hiyo ulipaswa kufanyika dar es salaam
lakini ukaahirishwa baada ya maoni ya wadau mbali mbali kushauri kuwa kwa kua
fainali itafanyikia dar es salaam basi ni vyema uzinduzi ukaanzia katika mikoa
ambayo itashiriki katika tuzo hizo ambapo kwa mujibu wa mapendekezo ya wadau mchakato
wa kuwapata washiriki wa tuzo hiyo utaanzia jiji Mbeya hapo tarehe 28.2.2016 sanjari
na kuwapata washiriki,
Dr.
Lawrence amesema tuzo hiyo itatolewa kwa watu ambao watakua wameonyesha mawazo
chanya ya namna ya kuisaidia Afrika iweze kupiga hatua za maendeleo,
Na
kwamba vigezo vya kushiriki katika tuzo hii dr.Lawrence alisema mtu
yeyote awe ni mwanamke au wanaume wenye umri kuanzia miaka kumi na sita
(16) na kuendelea anaruhusiwa kushiriki bila kujali kiwango cha elimu na kwamba
kinacho angaliwa ni fikra.
Akifafanua
zaidi kuhusu namna unavyoweza kushiriki alisema washiriki wanatakiwa kujaza
form maalumu ili waweze kupewa namba ya ushiri na kisha kisha watatakiwa kuwasilisha
live hotuba walio iandaa wakielezea “kwanini afrika pamoja na kua na
rasilimali za kila namna bado watu wake wangali masikini na tutafanyaje ili
tutoke hapa”?
Aidha
alisema kwa wale ambao wapo mbali lakini wangependa kushiriki katika shindano
hili pia wanaruhusiwa kushiriki na kwamba wao watalazimika kuandaa video clip
ya hotuba isiyozidi dakika 10 kisha kuiwasilisha wakielezea kwanini afrika pamoja
na kua na rasilimali za kila namna bado watu wake wangali masikini na
tutafanyaje ili tutoke hapa? Kisha ataituma clip hiyo katika whatsApp namba
0744- 683-511,
Lawremce
amesema washiriki wote wana ruhusiwa kutumia lugha ya moja wapo kati ya hizi
Kifaransa, Kiingereza au Kiswahili,
Na
kwamba kuna zaidi ya milioni mia tano (500m) zimetengwa kwa ajili ya shindano
hilo
washindi
watakabidhiwa tuzo ya kombe ambalo litakua ni ukumbusho wa ushiriki wake huku
wale watakao fikia kumi bora video clip zao zitaingizwa kwenye mfumo wa
dokumentari (documentary) kisha zitasambazwa katika nchi za afrika,
Dr.
Joshua alimaliza kwa kuelezea uzoefu wa taasisi hiyo ya Dream success
enterprises (njozi ya mafanikio) katika kuandaa tuzo mbali mbali nchini
ambapo alitaja baadhi ya tuzo ambazo zimewahi tolewa na taasisi hiyo kua ni
pamoja na tuzo ya SHUJAA KATI YETU ambapo mtunukiwa wa kwanza wa tuzo hiyo alikua
ni mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali bw. Ludovick Utouh ambae kwa
sasa amestaafu,
tuzo
nyingine ya SHUJAA KATI YETU ilitolewa mwaka jana 2015 kwa watu
watatu ambao ni Vicky Mtetema aliekua mtangazaji wa BBC alipewa tuzo
kutokana na ubunifu na ujasiri wake wa kupambana na kuhakikisha kuwa watu wenye
ulemavu wa ngozi(albino) wanapewa haki yao na kulindwa,
Saed
Kubenea alipewa tuzo ya umahili wa kuandika habari na kutumia kalamu katika
kuelimisha umma na mtu mwingine aliye pewa tuzo hiyo Mh. David Kafulila ambae
alipewa tuzo kutokana na ujarisi wake katika suala zima la kuhakikisha kwamba
watanzania wananufaika na rasilimali zilizomo hasa katika scandle ya ESCROW
Kwa maoni, swali na ushauri kuhusu tuzo hii piga namba
0744- 683-511 (namba hii ni maalumu
kwa ajili ya shindano hili na imesajiliwa kwa jina la MasterMind)
mbona hiyo fomu ya usajili wa kushiriki ilo shindano siioni au ndo muda umeisha?
JibuFutakama ipo naomba nitumiwe kwa gmail acount hii alexkatowo@gmail.com
JibuFutaahsanteee!!!!
Habari, Alex Katowo napenda kukufahamisha kuwa shindano hili lipo, lakini pia kwa maoni na ushauri kuhusu shindano hilo tafadhari piga simu namba 0744 683 511, namba hii imesajiliwa kwa jina la The MasterMind na ni maalumu kwa ajili ya shindano hili, ahasante kwa kuitembelea blog ya tuonane, tuendelee kushirikiana
Futa