Alhamisi, 18 Februari 2016

TAKWIMU ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

 




UFAFANUZI KUHUSU TAKWIMU ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo miongozo inayo simamia ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko na miongozo hii imetolewa na kusambazwa katika mikoa na wilaya zote nchini. Mwongozo huu unafuata utaratibu wa mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ujulikanao kama“Integrated Disease Surveillance and Response (IDSR)”

Katika mwongozo huu, taarifa za magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu pindi yanapotokea hutolewa taarifa mara moja kwa kutumia Ainisho sanifu yaani“Standard case definition”.

Aidha maainisho haya ya utambuzi waugonjwa yapo kwa ajili ya jamii (Community case definition) na katika ngazi ya kituo cha Afya (Health facility Case Definition).

Aidha utambuzi huu waainisho la awali, huzingatia dalili za ugonjwa ili mgonjwa aweze kupatiwa huduma wakati taratibu za vipimo zinapofanyika. Vipimo huchukuliwa kwa wagonjwa 10 wa awali wanao hisiwa kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu, na iwapo mmoja wao akithibitika kuwa na vimelea vya ugonjwa bas iuwepo wa mlipuko wa ugonjwa husika hutangazwa.

Aidha kutokana na utaratibu huu, ni wagonjwa wa mwanzo tu ndio watakao chukuliwa vipimo, na wengine watakao endelea kujitokeza huwa wanachukuliwa kuwa wanaugonjwa kwakuwa wana mahusiano na ushirikiano na wagonjwa waliokwishathibitika “epidemiological link”

Vipimo vya maabara  huchukuliwa tena kwa baadhi ya wagonjwa watakaoendelea kuugua ili kuweza kuangalia mwenendo wa ugonjwa husika na pia kupima usikivu wa Dawa (Antimicrobial Sensitivity Test).
Wizara inaendelea kusisitiza mambo mannemuhimu:-

1.   Utoaji wa taarifa ya wagonjwa wapya wa Kipindupindu huzingatia Ainisho Sanifu yaani Standard case Definition bila ya kuwepo uthibitisho wa ugonjwa kimaabara

2.   Pindi ugonjwa ukishathibitishwa kwa wagonjwa wa awalikumi (10) katika Mkoa/Wilaya/Halmashauri husika tayari mlipuko wa ugonjwa huu unathibitishwa na kutangazwa.

3. Uthibishwaji wa ugonjwa kima abara unafanyika tu kwa baadhi ya wagonjwa ili kuweza kuangalia mwenendo wa ugonjwa na pia kupima usikivuwa Dawa (Antimicrobial Sensitivity Test)

4.   Baadhi ya watu wenye ugonjwa wanaweza kupimwa na kuonekana kutokuwa na vimelea vya ugonjwa husika mfano kipindupindu. 

Zipo sababu nyingi zinazo weza kupelekea kipimo kutoonyesha uwepo wa vimelea hivyo mojawapo ikiwemo wagonjwa kuanza kutumia dawa kabla ya kufika katika vituo vyetu vya tiba.
Kwa mfano katika Mkoa wa Dar es salaam kwa siku kumi zilizopitakuanziatarehe 7 hadi 16 Februari,wagonjwa 16 wakipindupindu(Temeke 12 na Ilala 4) walikidhi vigezo vya ainisho sanifu na kupata matibabu katika kambi ya kipindupindu yaTemeke kwa wagonjwa waTemeke na Hospitali ya Amana kwa wagonjwa wa Ilala hivyo kulazimu kutolewa taarifa kwa mujibu wa muongozo.

Hitimisho
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ndio yenye dhamana ya kusimamia huduma za afya kwa wananchi hivyo Wizara itaendelea kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi kuhusu milipuko ya magonjwa ikiwamo kipindupindu. 

Viongozi wa Mikoa na Wilaya wanao wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi, mapema kwa kuzingatia miongozo na kwa wakati bila kuficha pindi wanapopata wagonjwa wapya. Vilevile jamii isiwekewe vikwazo vya faini au kunyanyapaliwa wapatapo ugonjwa huu kwani inaweza kusababisha wananchi kuogopa kwenda katika vituo vya afya. Wakuu wa Mikoa na Wilaya wawasiliane na Wizara iwapo kuna ufafanuzi wowote unaohitajika kwa taarifa zinazotolewa.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
17 JANUARI 2015

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni