muonekano wa jiji la Blantyre nchini Malawi |
muonekano wa Jiji la Blantyre - Malawi |
Wa
Tanzania waishio nchini Malawi wamezungumzia siku mia moja za Dr. John Pombe
Magufuli akiwa madarakani, wakizungumza kwa nyakati tofauti na ripota wa DW ambae
pia ni muandishi wa habari wa kituo cha
redio Galaxy kilichopo nchini Malawi bw. Ephraim Mkali Banda,
Wananchi
hao ambao ni wa fanyabiashara katika jiji la Blantyre Nchini Malawi wamesema
wanafurahishwa na utendaji kazi wa Rais
John Pombe Magufuli,
Faraja
Kyando anaeishi Nchini Malawi kwa ajili ya shughuli za biashara amesema anamshukuru mungu kwa kutupa kiongozi
bora ambae alikua ni hitaji wa watanzania kwa muda mrefu na hatimae amepatikana
huku akisema kuwa siku mia moja za utawala ya Dr. John Pombe Magufuli umeleta
matumaini makubwa kwa watanzania huku imani kubwa ikiwa ni kuzaliwa kwa
Tanzania mpya,
Pia
Faraja alibainisha sababu zinazopelekea watanzania kua na imani kubwa katika
utawala wa rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli kua ni namna rais alivyosimamia
zoezi la ukusanyaji wa mapato, alivyoweza kutimiza baadhi ya ahadi alizozitoa
katika kipindi cha kampeni kama elimu bure, kutatuliwa kwa migogoro ya ardhi
huku akitolea mfano kurejeshwa kwa mashamba makubwa ambayo yamekua chini ya
wawekezaji kwa muda mrefu jambo ambalo
limekua likipelekea migogoro ya mara kwa mara na ufuatiliaji wa muenendo wa utendaji kazi katika mahakama nchini, na
kuongeza kua mahakama ni miongoni mwa chombo ambacho kimekua kikilalamikiwa na
kungung’unikiwa na wananchi wa hali ya chini kutokana na kuto tenda haki mf
ucheleweshaji wa kesi, kuto tenda haki wakati wa hukumu nk,
Aidha
faraja alieleza namna anavyolichukulia suala la Rais anavowatimua kazi (kutumbua
majipu) baadhi ya watendaji ambao wanabainika kuto timiza majukumu yao kwa
mujibu wa sheria na kanuni za sheria za kazi, ambapo Faraja alisema anaunga
mkono utaratibu huo, na kufafanua kuwa rais yupo sahihi kuwatimua watendaji hao
kwani watendaji hao wamekua wakikata tawi walio likalia bila kujua mwisho wa
siku tawi likianguka na wao wataanguka aki maanisha kuwa kiongozi aliepewa
dhamana anaposhindwa kutimiza wajibu wake aliopewa kwa makusudi au kwa maslahi
binafsi ni sawa na kukata tawi alilokalia hivyo watendaji hao wanapo anguka
hawatakiwi kumlaum rais,
Mtanzania
mwingine anaeishi Malawi kwa shughuli za kibiashara katika mji wa SunSide
jijini Blantyre Nchini Malawi amesema tathmini yake juu ya siku mia moja za utawala
wa Dr.John Pombe Magufuli ni kua anaamini kuwa mungu amesikia kilio na maombi
ya watanzania na kuwapa walichokua wakikihitaji na hivo imani yake ni kwamba
Tanzania ya miaka 40 iliyopita inarejea tena kutokana na utendaji wa JPM, kwani
ni kiongozi ambae anauchungu na nchi yake pia wananchi wa hali ya chini
wanaokula mlo mmoja
Akizungumzia
timua timua ya rais dhidi ya watendaji
wabovu alimaarufu kama (kutumbua majipu)
hali ambayo imekua gumzo nchini na hata katika nchi nyingine jirani na
kusababisha hisia tofauti huku wengine wakimtafsiri Rais kua ni udikteka na
wengine wakisifia kua ni uongozi bora uliotukuka ,
mfanya
biasha huyo amesema hashangazwi na suala hilo kwa kua hata katika ngazi ya
familia watoto wanazeza kumwita baba dikteta kutokana na utaratibu anaotaka
kwenda nao huku akitolea mfano kuwa hadhani kama kuna baba ambae anaweza
akakubali mtoto afanye mambo nje ya matakwa yake hivyo hata hao wanaomsemea
vibaya na kubeza kasi ya Rais Magufuli ni dhahiri kua nao ni sehemu ya majipu
na vijipu kwa kua Rais huwatimua watendaji wabovu na wazembe.
Rais wa awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli |
Blog hii inatoa shukrani nyingi kwa Ephraim Mkali Banda repoter wa
Dw, kwa kufanya mahojiano hayo na Watanzania waishio Malawi kwani hii huonyesha
ni jinsi gani sasa watanzania wanajivunia utanzania wao na wanafurahia kuwa
watanzania kwani tumeshuhudia siku za nyuma baadhi ya watanzania hususani
vijana walio kata tama wakijutia kua watanzania na kulazimika kutumia misemo
mbali mbali inayowakilisha hisia zao kama “ni
bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuwa binadamu Tanzania”
Hari hiyo safi sana huo ndio uhusiano nzuri wa wana habari
JibuFutaahsante kwa maoni yako Hawa Ahmed, ahsante kwa kuitembelea blog hii ya tuonaneblog, tuendelee kushirikiana
Futa