HABARI KUTOKA MALAWI NA EPHRAIM MKALI BANDA.
Picha hawa ni baadhi ya wakimbizi hao kutoka Msumbiji wakiwa katika picha tofauti
Nchi ya Malawi imewapokea
wakimbizi wengine zaidi ya 8000 kutoka inchi ya Msumbiji, Wananchi hao raia wa Msumbiji wana kimbia nchi
yao baada yakuzuka mapigano ya kisiasa kati ya wafuasi wa chama tawala cha
Frelimo na Renamo, chama cha Renamo hakikubaliani na matokeo ya uchaguzi ambayo yalitangazwa nchini humo.
Idadi hiyo ime thibitishwa
na shirika la kuhudumia wakimbizi duniani (UNHCR). Shirika hilo limeipongeza
serikali ya Malawi kwa kua pokea wakimbizi hao,
Pia Shirika hilo limetoa
tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza tokea kutokana na kuwepo
kwa idadi ya watu wengi katika kempu ya Kapise iliyopo katika wilaya ya Mwanza
mpakani na Msumbiji.
Umoja wa mataifa umesema
Dola milion kumi na tano (kwacha Trillion moja ya Malawi) inahitajika ili
wakimbizi hao waweze kupewa msaada wa kutosha.
Nao mabalozi wa nchi za
Ujerumani na Brazil balozi Peter Woesta na Gustavo Nogueira walio tembelea
kempu hio kujionea hali halisi ya wakimbizi.
UNHCR imeiomba serikali ya
Malawi kufikiria namna ya kuongeza eneo lingine kwa ajili ya wakimbizi ambao wana
endelea ku miminika katika nchi hio.
Serkali ya Malawi imesema
inafikilia ombi hilo. Takribani wakimbizi elufu shirini na tano kutoka Msumbiji
wanahifadhiwa nchini Malawi. Watu wengine wamesema Umoja wa Africa unatakiwa
kuangalia hali inayotokea kwa sasa Msumbiji kwa upana zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni