Wanakijiji waliofika katika zahanati ya Uturo kumsikiliza katibu mkuu wa wizara hiyo |
Katibu
mkuu wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto dkt.Mpoki
Ulisibusya akimueleza jambo mwenyekiti wa kijiji cha Uturo bw.charles
mtambalike wakati akikagua mazingira ya zahanati ya uturo
Kaimu
mkurugenzi msaidizi kitengo cha huduma za uzazi na mtoto toka wizara ya afya
dkt.Georgina Msemo akiongea na wananchi wa kijiji cha Utoru,
|
Dkt.Mpoki
akionesha moja ya bango lililomvutia kwenye zahanati hiyo ambalo linaonesha
maudhurio ya kliniki kwa mama na baba,aliyekaa mbele ni kaimu mganga mkuu wa
wilaya ya Mbarali dkt.Hance Mpumilwa
Jamii
imetakiwa kuhakikisha vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi kwa akina mama
wajawazito na watoto nchini vinatokomezwa.
Hayo
yamesemwa leo na katibu mkuu wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na
watoto dkt.Mpoki Ulisubisya alipotembelea zahanati ya kijiji cha uturo
kilichopo wilayani Mbarali ambacho wananchi wa kijiji hicho wanashiriki moja
kwa moja katika kuondoa matatizo hayo.
Dkt.Mpoki
alisema serikali katika kutekeleza sera ya afya nchini inahakikisha akina mama
wajawazito na watoto wachanga hawafi kwa magonjwa yanayozuilika "Gharama
za afya zimekuwa Kubwa sana, hivyo nguvu yetu na umoja ndiyo njia pekee ya
kujikomboa na kuleta maendeleo ya nchi na kutokomeza vifo vya akina mama nchi
nzima"alisema
Aidha
aliwataka wananchi kujua afya ni wajibu wa kila mtu na inawezekana endapo kila
mtu atajitolea kuhakikisha huduma za kiafya zikiwemo za kliniki na tabia ya
kuzalia nyumbani zinaachwa.
Hatahivyo
katibu mkuu huyo aliitaka mikoa mingine kufika kijijini hapo kujifunza ni jinsi
gani wamefanikiwa kuwashirikisha wananchi wote hususan akina baba kushiriki
kuanzia ujauzito hadi mtoto anapozaliwa,
Naye
mkuu wa zahati hiyo Tabibu Wilson Chotamganga alisema kijiji hicho kimefanikiwa
kutokomeza vifo hivyo kwa kuunda timu ya viongozi wa Vitongoji wa huduma za
uzazi na mtoto pamoja na kuanzisha madaftari mawili ya akina mama wajawazito na
watoto chini ya miaka mitano na kukubaliana sheria ndogodogo za kutozwa
shilingi elfu tano kwa yeyote atakayekiuka makubaliano na taratibu zilizowekwa
Zahanati
ya Uturo iwe ya mfano kwa kutokuwa na vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na
uzazi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni