Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali akizungumza katika kikao cha wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto). |
Katibu wa wazee wa Dar es Salaam Mohamed Mtulia (Kulia) akizungumza wakati wa kikao Mhe. Ummy mwalimu (kushoto) na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali. |
Kaimu kamishna Ustawi wa Jamii Rabikira Mushi akizungumza katika kikao cha wazee wa Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga. |
Serikali imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria
itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili
kwa sasa.
Mpango huo umetolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na baadhi
ya viongozi wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam alipokutana nao mapema wiki hii
ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe.
amesema wazee wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku
nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata
mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na
uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.
“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa
kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bunge mwezi Septemba
ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza
masuala yahusuyo wazee” Alisema Mhe.Ummy.
Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed
Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa
kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto
zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya
wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.
Aidha Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo
chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa
huduma kwa wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha
wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya
katika maeneo mengi zaidi.
Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba
kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kujadili mshtakabali wa
maendeleo ya wazee nchini.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni