Jumatatu, 4 Aprili 2016

Mkuu wa Mkoa Mbeya, arejesha hekta 5000 kwa wananchi wa kijiji cha Luhanga, aagiza watendaji wachukuliwe hatua kwa kugawa ardhi kwa muwekezaji kinyume cha sheria

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali, katika mkutano wa hadhara hapo jana
Baadhi ya wananchi na waliojitoke kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wakiwemo waandishi wa habari

Hekta 5000 za ardhi ya wananchi wa kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali zilizokuwa zimetolewa kwa wakulima zaidi ya 200 wa chama cha Luhanga (Luhanga AMCOS),

Serikali imetoa agizo hilo huku ikiuagiza uongozi wa halmashauri kuwachukulia hatua watendaji wote walihusika na mchakato wa ugawaji wa ardhi hiyo.

Akikabidhi ardhi hiyo jana, kwa wananchi wa Kata ya Luhanga, Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala, alisema serikali imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kwamba zoezi hilo lilifanyika kinyume na sheria na kanuni za ardhi ya mwaka 1999 za vijiji zinavyoelekeza na kwamba halmashauri ya kijiji haina mamlaka ya kugawa ardhi zaidi ya ekali 20 hadi 50

Aliongeza kua licha ya ugawaji wa ardhi hiyo wawekezaji hao wamebainika kua ni wababaishaji kutokana na kushindwa kutekeleza kile walichokiahidi kwa wananchi kuhusiana na maendeleo kwa wakazi wa eneo husika

Amesema mkoa wa mbeya unajulikana kwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi hususani wilaya ya mbarali hivyo yeye kama mkuu wa mkoa atahakikisha anashughulika vyema na suala hilo.

kwa upande wa baadhi ya vijana walio hudhuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa wamempongeza mkuu wa mkoa kwa maamuzi hayo hivyo wakamuahidi kua kufuatia maamuzi hao wao kama vijana watahakikisha wanaitumia ardhi hiyo na kuacha kujihusisha na  mchezo wa pool na michezo mingine nyakati za kuwajibika na kwamba walikua wakilazimika kufanya hivyo kutokana na kukosa majukumu ukizingatia vijana wengi amejiari katika kilimo hivyo suala la kunyang’anywa ardhi liliwaathiri,

Hata hivo Mkuu wa Mkoa Mh, Amosi Makala ametoa rai kwa viongozi kua hakikisha kua wanatenda haki kwa wananchi wote katika zoezi la ugawaji ardhi hiyo iliyorejeshwa mikononi mwa wananchi huku akionya viongozi kuto jihusisha na vitendo vya rushwa katika zoezi hilo,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni