Waziri.wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto akisalimia na watumishi mara alipofika kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa |
waziri Ummy akimsalimia mtoto jenifer Joel(9) mkazi wa chunya aliyelazwa hospitalini hapo. |
Hospitali ya Meta imetekeleza maagizo ya Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto ya kutoa kipaumbele kwa wazee wote nchini wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma |
waziri wa afya akiwasalimia wagonjwa waliofika hospitali ya uzazi ya meta kupata matibabu |
Hospitali zinazotumia mfumo wa
ukusanyaji mapato wa kielectroniki wametakiwa wasibweteke na mapato
wanayoyakusanya kila siku.
Rai hiyo imetolewa na waziri wa
afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu wakati
alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda ya mjini Mbeya,
Ummy amesema ukusanyaji wa mapato
kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma za afya
nchini ikiwemo ununuzi wa dawa,vifaa na vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha
kwa watumishi
"Bado tunatambua hali ya
uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote, tukiweza
kusimamia vizuri hili tutafanikiwa" alisema mh. Ummy
Aidha amesema wanatarajia katika
serikali ya awamu hii bajeti ya dawa itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha
na bajeti za nyuma, hivyo wameishauri bohari kuu ya dawa wanunue dawa toka kwa
wawekezaji wa hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na
upatikanaji wa dawa kwa haraka.
Waziri Ummy Mwalimu ameutaka Mkoa
kufuatilia, kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi
wa dawa
"Tunao watumishi wachache wa afya ambao
wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka kwenye maduka ya dawa binafsi, hao
hatutowafumbia macho na kuwapeleka mahakamani"
Kuhusu upungufu wa watumishi wa
kada ya afya nchini ,Waziri wa afya amesema, nchi ina upungufu wa asilimia 52
hivyo serikali inatarajia kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni
ambao watatawanywa nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni Katika hospitali ya
uzazi ya Meta,
Aidha waziri huyo ameguswa na
ufinyu wa wodi za wazazi na kupelekea wakina mama wajawazito na waliojifungua
kulala chini na wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya
haraka ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa akina mama wajawazito
na watoto njiti.
Hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya inakusanya
kwa mwezi kiasi cha shilingi milioni mia
tano, inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu milioni mbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni