Jumanne, 7 Juni 2016

Serikali ya Kenya yafanya kikao cha dharula jioni hii na waandishi wa habari yapiga marufuku maandamano!!

Serikali ya Kenya imepiga marufuku maandamano ya aina yoyote nchini humo, kufuatia vifo vya watu kadhaa, baada ya ghasia kukumba taifa hilo la Afrika Mashariki, yaliyoandaliwa na muungano wa upinzani CORD.
Hayo yamesemwa hivi punde na waziri wa usalama wa ndani nchini humo, Bwana Joseph Nkaissery, katika kikao na wanahabari.
Bwana Nkaissery anasema hayo ni kutokana na waandamanaji kubeba silaha butu na mawe wakisababisha uharibifu mkubwa na kuhatarisha usalama wa taifa.
Hatua hiyo inafanyika saa chache tu, baada ya mahakama nchini humo kuupa upinzani uhuru wa kuandamana.
Katika mkutano huo walikuwepo mkuu wa Sheria na kamanda mkuu wa polisi nchini Kenya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni