Jumatano, 22 Juni 2016

Waziri Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na ugonjwa usio julikana!!

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto akiwasalimia wagonjwa hao kwenye hospitali ya wilaya ya Kondoa.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.

Katika ziara hiyo ameambatana na wataalam mbalimbali ambao wameweka kambi kwenye vijiji hivyo ili kufuatilia wagonjwa majumbani.

Vile vile ametembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.

Waziri wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na wanakijiji wa mwaisabe(hawapo pichani)
Mbunge wa Kondoa Mhe. Juma Nkamia akizungumza na wanakijiji hicho.

Wanakijiji wakimsikiliza waziri Ummy Mwalimu(hayupo pichani)

Waziri Ummy mwalimu akiwajulia hali wagonjwa waliokumbwa na ugonjwa usiojulikana.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto akiwa na wataalam mbalimbali watakaofanya uchunguzi wa chanzo wa ugonjwa huo.
Hapo jana tarehe 21/6/2016  vituo mbalimbali na mitandao ya kijamii viliripoti vijiji hivyo kukumbwa na ugonjwa usio julikana ambapo hadi jana taarifa ziliarifu kua watu 7 na wengine 21 walilazwa baada ya kuzuka kwa ugonjwa huo ambao hadi sasa madaktari hawajua tiba yake
Dalili za ugonjwa zilielezwa kua ni pamoja na kutapika, kuharisha, ngozi na macho kuwa ya njano pamoja na kuumwa na tumbo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni