Rais Magufuli akizungumza katika hafla ya kiapo cha uadilifu cha Wakurugenzi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam July 12,2016. |
Rais Magufuli
amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara TAMISEMI kuwafukuza kazi baadhi ya vigogo wa Tamisemi, pia aeleza sababu zilizopelekea kuamua Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) kuwa chini yake.
Kizungumza
wakati wa hafla ya kula kiapo cha uadilifu kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Majiji
na Miji iliyofanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam jana tarehe 12/7/2016, Magufuli
amesema kuwa amelazimika kufanya hivo kwa kuwa alibaini utaratibu uliokuwa
ukitumika kuwapata wakurugenzi katika miaka ya nyuma ilikuwa na udanganyifu
mkubwa sana huku vitendo ya rushwa vikichukua nafasi zaidi.
Amesema alibaini kuwa vitendo hivyo vya kutumia rushwa ili kupata
ukurugenzi vilikuwa ni mazingira yaliyotengenezwa na baadhi ya vigogo wa
TAMISEMI kwa maslahi yao binafsi.
Aidha alisisitiza kuwa nafasi ya Ukurugenzi ni nafasi muhimu sana
katika kujenga uchumi wa wananchi hasa wananchi wa chini hivyo umakini mkubwa
umetumika kuwateua wakurugenzi hao kutokana na umuhimu wao ambapo alisema hatua
za uteuzi zilikuwa na umakini mkubwa na
kwamba zoezi la uteuzi huo limechukua miezi nne (4) hadi kuwapata wakurugenzi
hao.
Baada ya kusema hayo Magufuli aliongeza kuwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara Tamisemi
awaondoe vigogo wote ambao wamekua wakijihusisha na vitendo vya rushwa kwani
anawafahamu vema.
Hata hivyo Rais Magufuli amesema amekuwa akifuatilia na kusoma
taarifa katika mitandao ya kijamii na amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya
mitandao kutoa taarifa ambazo zimekua zikilenga kupinga uteuzi ama kuwachafua
baadhi ya viongozi walioteuliwa kwa madai kuwa hawana sifa ambapo alisema yafuatayo “kutokana na hilo nimejifunza
kitu, ukiona unashangiliwa na adui rudi nyuma ujiulize umekosea wapi, ukiona
unasemwa adui jua umewatwanga”
Rais Magufuli alisisitiza kuwa katika uteuzi huo amejiridhisha na hajabahatisha
na anaimani kuwa wakurugenzi hao wataenda na kasi anayoitaka na kuijenga
Tanzania anayoitaka ambapo aliwasifu kuwa wengi wao ni wasomi wenye diploma,
degree na master.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni