Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Bw. Modest Nkulu wakati akitoa tamko. |
Chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (MBPC) kimeeleza kuto kuwa na imani na hukumu
iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Mbeya baada ya kumwachia huru Herman Joseph mwenye (33) dereva wa gari lenye
namba za usajiri T,321 CDA aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Shanta
Mining, ambaye aliwagonga waandishi watatu
ambao walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya King Loin yenye namba za
usajili Mc 923 AZQ uliyo kuwa
ikiendeshwa na Gabriel Kandonga wakati wakitekeleza majukumu yao ya kikazi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya
kuto ridhishwa na mwenendo wa kesi pamoja na hukumu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari
Mkoa wa Mbeya (MBPC) ndugu Modestus
Nkulu amesema ajali hiyo ambayo ilitokea mnamo tarehe 31/8/2016 katika barabara
ya kutoka Mbalizi kuelekea Mkwajuni chunya ikihusisha gari aina ya Toyota Land
Cruiser mali ya Shanta Maning na pikipiki ambayo ilikuwa ikitumiwa na
waandishi wa habari ndugu Gabriel Kandonga, Ibrahim Yasin na Aines Thobias.
Mwenyekiti Nkulu amesema baada ya ajali hiyo, mnano tarehe
31.8.2016 kesi yenye kumbukumbu namba
MB/TR/RB/3828/2016 ilifunguliwa katika kituo cha mbalizi (Wilaya ya kipolisi
Mbalizi) ambapo katika upelelezi ilishughulikiwa na WP 5830 CPL LUCY na
mchoraji wa ramani ya ajali G 3944 PC MUSA wakati mkaguzi wa vyombo vya moto
VIHECLE INSPECTOR wa polisi E 4677 CPL HAJI huku kesi iliyo sajiliwa kwa namba
108/2016 iliendeshwa na kusikilizwa chini ya Hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya
Zawadi Laizer na wakili wa serikali Catherin
Paulokwa.
Aidha Nkulu akaeleza mazingira yaliyopelekea wanahabari
mkoani Mbeya kukosa imani na mwenendo wa kesi pamoja hukumu iliyotolewa mnano tarehe 13/12/2016 na
mahakama hiyo ni kuendesha kesi bila mashahidi muhimu(wahanga wa tukio) kuitwa
mahakamani, ambapo Nkulu alisema kufika kwa wahanga mahakamani kungesaidia
mahakama kuona hali za majeruhi pamoja na uhalisia na ukubwa wa kosa.
Akifafanua zaidi mwenyekiti Nkulu amesema kuwa baada ya
hukumu hiyo kutolewa uongozi wa chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa mbeya
ukiongozwa na Modest Nkulu ambae ni Mwenyekiti wa Mbeya Press Club mnamo tarehe 14/12/2-16 ulilazimika kubisha
hodi katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ndugu Joseph Pande ili
kuwasilisha masikitiko yao dhidi ya mwenendo wa kesi pamoja na hukumu
iliyotolewa.
Aidha anaongeza kuwa baada ya kufanikiwa kufanya mazungumzo
na mwanasheria mkuu wa mkoa wa mbeya ndugu Joseph Pande na kueleza masikitiko
yake kuanzia mwenendo wa kesi tangu polisi, ofisi ya mwanasheria na mahakama,
mwanasheria huyo alikiri ofisi yake kupokea taarifa ya upande wa mashitaka
kushindwa hivyo ofisi yake imejipanga kushughulikia suala hilo kwa kukata
rufaaa kupinga hukumu hiyo.
Hata hivyo katika kupinga hukumu hiyo chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Mbeya na wanachama wake walikuwa na tamko rasmi
linalo ashiria kupiga hukumu hiyo likieleza maneno yafuatayo “Kwa umoja wetu kama waandishi wa habari mkoa
wa Mbeya, tunapinga hukumu hiyo, kwa kuwa tunahisi haijazingatia haki na usawa
kwa wahusika wote hususani wa jamhuri ambao ni walalamikaji”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni