![]() |
Wananchi wa mtaa wa simu manispaa ya Kigoma ujiji wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa huo Tausi issa wakishinikiza kukomeshwa kwa vitendo hivyo. |
Mapema wiki hii hali ya sintofahamu ilizuka kwa wakazi
wa maeneo kadhaa ya katika Manispaa ya
Kigoma Ujiji baada ya kuibuka kwa kundi la kihalifu la vijana alimaarufu kama teleza ambao huvamia nyumba ambazo
huishi wanawake na kuwabaka nyakati za usiku
Inadaiwa vijana hao maarufu kama teleza, hujipaka
mafuta ya mawese kabla ya kuvamia nyumba za ambazo huishi wanawake pekee kisha kutenda
uhalifu huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Kigoma,
Ferdinand Mtui alithibitisha kuwapo matukio hayo na kusema tayari jeshi la
polisi limemkamata mtuhumiwa mmoja baada ya kuwahoji wanawake nne (4) waliofika
kituo kikuu cha polisi kutoa malalamiko ya kuingiliwa katika nyumba zao na
vijana hao.
Hata hivyo, Kamanda Mtui aliwatoa wasi wasi wakazi wa
Manispaa ya Kigoma Ujiji akieleza kuwa vitendo vinavyofanywa na vijana hao
havihusiani kwa namna yoyote na vitendo vya kishirikina.
Alisema wanaoviendesha ni watu halisi ambao wameamua kufanya
vitendo hivyo na polisi imeanza kuchukua hatua madhubuti za kupambana navyo.
Inaelezwa kua kufuatia hali hiyo kundi la wanawake
walikusanyika kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Simu Kata ya Mwanga Kusini
wakishinikiza serikali kuchukua hatua.
Ambapo katika maelezo yao walidai kua
tayari wanawake wanne walijeruhiwa miili yao kwa silaha ambazo wabakaji hao
wamekuwa wakitembea nazo baada ya kuvamia nyumba zao.
Diwani wa kata ya Mwanga Kusini, Mussa Maulid alikiri
kupokea malalamiko ya wanawake 12 wanaodai kuingiliwa na vijana hao maarufu
kama teleza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni