Na.Catherine Sungura-Monduli
Wilaya ya Monduli inatarajia kutoa kingatiba ya
ugonjwa wa trakoma(vikope) kwa watu wapatao 140,962 kwa ngazi ya jamii
kaya kwa kaya hadi ifikapo mwezi julai mwaka Huu
Haya yamesemwa leo na mkuu wa wilaya ya Monduli
Fransic Miti wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji dawa katika kijijo cha
Losingirani.
Miti alisema kila mtu yupo katika hatari ya kupata
maambukizi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele"napenda
kusisitiza kila mwanajamii ahakikishe kila mtu katika familia anatumia dawa hizi
ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi ambayo ni tayari katika jamii yetu.
Aidha aliahidi kulisimamia zoezi hilo ipasavyo
katika ngazi zote kwani vifaa vyote vya utekelezaji wa zoezi hili
vimeshawafikia katika wilaya Nzima.
Mkuu wa Wilaya alisema kwa mwaka uliopita wilaya
yake imetekeleza zoezi la ugawaji wa dawa za kudhibiti magonjwa ya
kichocho na minyoo ya tumbo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kwa
ufanisi mkubwa ambapo kati ya watoto 29,427,watoto 28,205 walipatiwa kingatiba
ambayo ni sawa na asilimia 95.8
Hata hivyo alisema kwa zoezi la mwezi wa tano
mwaka huu la umezaji dawa za minyoo zilitolewa kwa watoto 31,150 sawa na
asilimia 97.3 kati ya watoto 32,000.
Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti
Magonjwa Yaliyokuwa
Hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Upendo Mwingira alisema maambukizi ya
ugonjwa wa vikope(trakoma) upo kwa kiwango cha juu kwenye maeneo ya wafugaji
ambapo asilimia 57 ya watu waliofanyiwa utafiti mwaka 2004 hadi 2006 ilionesha
wana tatizo la vikope hasa wilaya ya Monduli,Longido pamoja na Ngorongoro.
inakadiliwa hadi kufikia mwaka 2020 dunia nzima
iwe imetokomeza ugonjwa huu kwa kugawa dawa ambazo ni tiba na kinga.
![]() |
Mwenyekiti wa kijiji cha Meserani juu,Ngimasirwa Silalee akimeza dawa kwenye uzinduzi huo,kulia ni mkuu wa wilaya ya monduli |
![]() |
Wananchi wa kijiji cha Meserani wakisikiliza hotuba toka mkuu wa wilaya (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa umezaji wa kingatiba za ugonjwa wa trakoma uliofanyika kwenye kitongoji cha Losingirani |
![]() |
Diwani
wa kata ya Meserani Mhe.Loti Naparana akimeza kingatiba ya
Trakoma(Zithromax)wakati wa uzinduzi huo |
![]() |
Mama wa boma bi.Himayo Merio (aliyeshika kikombe)akipokea kingatiba toka Kwa mhudumu wa afya ngazi ya jamii bi.Jamila Karanga.zoezi hili linafanyika katika jamii hiyo kwa kuwatembelea kaya kwa kaya |
![]() |
Mmoja wa mtoto katika boma la mzee Sanare Midimi wa kitongoji cha Losingirani akinyweshwa dawa iliyopo kwenye mfumo wa maji maalum kwa watoto wadogo(Picha zote na Catherine Sungura-Wizara ya Afya) |
![]() |
Dkt.Upendo
Mwingira(mwenye nguo burgundy) akimpatia kingatiba Mkuu wa Wilaya ya Monduli
Francis Miti |
![]() |
Kikundi cha ngoma cha akina mama wajasiriamali cha kimasai wa kijiji hicho wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa umezaji wa kingatiba ya Trakoma |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni