
Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ubakaji mkoani iringa,
serikali imelazimika kuwagiza wazazi za
walezi kuto ruhusu watoto wenye umri chini ya miaka 14 kutembea mitaani haswa
nyakati za jioni kuanzia saa 12 jioni.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Iringa ndugu Richard
Kasesela, ambapo amesema kua wazazi na walezi wana jukumu la kuwalinda watoto
dhidi ya ukatili ambao unakua kwa kasi mjini Iringa.
Inaelezwa kua watekelezaji wa matukio hayo ya ukatili dhidi ya
watoto kama ubakaji na ulawiti wamekua wakitumia mbinu ya kuwahadaa watoto kwa
kuwapa kiasi kidogo cha pesa ama kujifanya wakiwatuma katika maeneo ambayo ni
rahisi kwenda kuwafanyia ukatili huo.
Wiki moja iliyopita wananchi walimpiga hadi kumuua kijana
aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel (25-30), baada ya kukutwa akimbaka
mtoto mwenye umri wa miaka kumi, katika eneo la Mtwivila, Manispaa ya Iringa.
katika kipindi cha miezi mitatu kumeripotiwa matukio zaidi ya 30
ya ubakaji katika Manispaa ya Iringa huku watuhumiwa kumi na saba (17) wakiwa
wamekamatwa na kutiwa mbaroni
Kasesela amesema matatizo ya ubakaji na uwalawiti watoto
yamekuwa sugu hivyo hili kukomesha hali hiyo ushirikiano baina ya polisi, wananchi na
viongozi wa serikali na dini unahitajika ili kukomesha hali hiyo.
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa ndugu Joseph
Lyata amesema tatizo la kushamiri kwa
vitendo ya ubakaji na ulawiti vinachangiwa na imani za kishirikina,
Alisema katika uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwepo kwa imani za
kishirikina baada ya kubaini kumekua na vikaratasi vilivyokuwa vikisambazwa
mitaani vikishauri wanaume kujihusisha na vitendo hivyo vya kikatili sambamba
na kujiunga na freemason ili kufanikiwa
kimaisha.
“Mtaa wa Semtema ndiyo
ulikuwa tishio na huko tuliokota vikaratasi vilivyokuwa vimeandikwa ukitaka
kutajirika, jiunge na freemason pia ubake au kulawiti mtoto chini ya miaka 14,” alisema.
Lyata alisema sababu nyingine ni ulevi wa kupindukia na utumiaji
wa dawa za kulevya kama bangi.
Alisema kukithiri kwa vitendo hivyo kumeifanya manispaa hiyo
kutangaza jambo hilo kuwa ni janga ambalo lazima wapambane nalo kwa kuwasaka
wabakaji.
Aliongeza kua vitendo vya ulawiti na ubakaji vimekua vikifanywa
hata majumbani na kwamba kufuatia hali hiyo serikali imeanza kuawambua wtoto wa
mitaani na kuwarudisha majumbani kwao ili kuwanusu na vitendo hivyo.
Mmoja kati ya wananchi aliejitambulisha kwa jina la Gerald
Matibabu alisema kwa upande wao wananchi sasa wamekua wakijichukulia sheria
mkononi kwa kuwa ua wale wote wanaobainika kujihusisha na vitendo ubakaji na
ulawiti.
Hata alisema wamelazimika
kujichukulia sheria mkoni kwa kua watuhumiwa wamekua wakiachiwa huru na polisi
na kurejea mtaani jambo ambalo linawaumiza sana wananchi
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, John Kauga alikiri kuwapo
kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji na kuwataka wananchi kutoa taarifa haraka
vinapotokea.
“Kuna matukio mengi pia majumbani, wazazi wasifiche, watoe
taarifa kwa polisi ili hatua kali za kisheria zichukuliwe,” alisema.
Aliwataka wananchi kupinga imani za kishirikina
zinazowahamasisha kufanya ukatili kwa watoto kwa madai ya kutajirika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni