Jumapili, 27 Novemba 2016

HIFADHI YA TAIFA UDZUNGWA YACHANGIA MADATI 1062 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 128.

Kushoto ni Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha, akizungumza na wanahabari hivi karibuni.

Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha,  akiwaelezea jambo waandishi wa habari (hawapo pichani)


Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha mesema kuwa Hifadhi ya Taifa Udzungwa imechangia jumla ya madawati 1062 yenye thamani ya sh. 128 milioni katika shule  za msingi 18 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu Wilayani Kilombelo Mkoani Morogoro.

Akizungumza na wanahabari wanawake kutoka katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania ambao walitembelea hifadhi hiyo ya Udzungwa, Simon amesema hifadhi hiyo imechangia kiasi hicho cha madawati kupitia mradi wa Ujirani Mwema  na kwamba  madawati hayo yametolewa kwa awamu tatu.

Akafafanua zaidi kuwa awamu ya kwanza Tanapa ilichangia madawati 414 yenye thamani y ash. 56 milioni madawati hayo yalipelekwa katika shule za msingi 17 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu, awamu ya pili madawati 278 yenye thamani ya sh.26 milioni ambayo tayari yamesha kabidhiwa katika shule za msingi 18 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kitatu , na awamu ya tatu ni madawati 370 yenye thamani y ash. 46 milioni ambayo yatakabidhiwa hivi karibuni baada ya kukamilisha taratibu za kukabidhi kwa shule  18 ambazo zipo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu Wilayani Kilombelo mkoani Morogoro.
  
Navasha akaongeza kuwa  TANAPA ilianza mchakato wa kuchangia madawati katika vijijini vinavyopakana na hifadhi ya Udzungwa tangu mwaka 2013 ambapo alibainisha kuwa miongoni mwa vigezo ambavyo vinatumika katika kuchagua ni kijiji ama shule gani zipewe madawati  au miradi mingine yenye lengo ya kuwasaidia wananchi waishio katika vijiji vinavyo pakana na hifadhi  hiyo ni pamoja na kuangalia vijiji ambayo vimekuwa vikitii sheria za uhifadhi bila shuluti kama kushiriki kutoa taarifa za ujangili, kuto kata miti, kuto choma moto,  kutofanya shuhuli za uwindaji ndani ya hifadhi nk.

Hata hivyo Naivasha amesema kuwa ipo miradi mingi ya ujirani mwema,  miongoni mwa miradi hiyo ni pamoaja na ujenzi wa vyumba vya madarasa,ufugaji wa kuku hususani kwa wakina mama, ufugaji nyuki, ufugaji ngombe na mbuzi, ambapo miradi ya ufugaji imeanzishwa katika maeneo ambayo wakazi wake hususani wanaume walikuwa wakijihusisha zaidi na shughuli za uwindaji ndani ya hifadhi.

Naivasha amefafanua kuwa dhumuni la kuanzisha miradi ya ujirani mwema ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa ni kuondoa migogoro baina ya wakazi waishio maeneo ya karibu na hifadhi na Tanapa, kuimarisha kudhibiti wa vitendo vya ujangili,  kwani kupitia miradi hiyo Tanapa inapata nafasi ya kutoa elimu kwa wananchi kila inapobidi kufanya hivyo.

Akizungumzia changamoto ambayo Tanapa inakumbana  nayo katika kutekeleza miradi hiyo ya ujirani mwema, ‘’changamoto kubwa tunayo kabiliana nayo ni ugumu wa wananchi kuchangia ile asilimia ndogo wanayopaswa kuchangia, mnajua kwa kawaida Tanapa tunachangia 70% na wananchi nao wanatakiwa kuchangia 30% lakini wanakuwa wagumu kutoa” alisema Naivasha.

Kuhusu sababu zinazopelekea wananchi hao kuwa wagumu kuchangia hata kwa kiasi kidogo wanachopaswa kuchangia Naivasha amesema ni matumaini makubwa ya wananchi. “unajua wananchi wengi wanaamini kuwa Tanapa ina hela nyingi sanaa pia hela hizo zinatolewa na serikali, hivyo kuna tunapata changamoto kubwa sana tunapoenda kukabidhi miradi hiyo ukiwaambia wanatakiwa kuchangia wanaona kama wewe ulieenda kukabidhi  mbaya hivyo wananchi wanamatumaini makubwa kupita kiasi hiyo ndiyo changamoto” alisema Naivasha.


Alimaliza kwa kutoa wito kwa wananchi waishio maeneo jirani na hifadhi kutambua kuwa jukumu la kuzilinda hifadhi nila kila mwananchi pia akawataka washiriki vema katika kuisaidia Tanapa kupambana na vitendo vya kijangili ambavyo vinashamiri kwa kasi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni