Jumatatu, 5 Desemba 2016

Waziri Mpina aeleza kitakacho ifanya Serikali ya awamu ya 5, isiyumbe wala kuyumbishwa!!


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa Kinziga, Salasala Jijini Dar es Salaam.

NAIBU  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema Serikali ya awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za Mungu katika kuwatumikia wananchi wake na si vinginevyo.


Pia amesema  Serikali ya awamu ya Tano kamwe haitayumbishwa wala kuyumba katika kutenda yaliyomema kwa maendeleo ya nchi  kwa kuogopa maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kusifu  na Kuabudu na kuliombea Taifa la Kanisa la Tanzania Assemblies  of God lililopo katika eneo la Kinzugi Salasala, alisema  Serikali itaendelea kusimamia misingi yake bila kuogopa maneno ya watu wanaoyoikatisha tamaa kwani Sheria na Katiba za nchi zinatokana na maneno yaliyopo  katika vitabu vya Mungu.
Alisema watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwaombea viongozi katika kutenda kazi zao kwani uongozi waliokuwa nao ni uchaguzi kutoka kwa Mungu na sio kwa nguvu za mtu yeyote.

" Uongozi unatokana na  Mungu,Mimi Mpina sikujua kama ningekuwa Waziri nilimaliza siku mbili sikujua kama niliteuliwa kuwa Naibu Waziri kipindi hicho  nilikuwa shambani nikafatwa na kuambia kuwa nimechaguliwa ,nikasema ni uweza wa Mungu,"alisema na kuongeza kuwa
"Utawala wa awamu ya tano tunemtanguliza mbele Mungu,tunaomba muendelee kutuombea tutekeleze majukumu yetu licha ya kuwepo kwa vikwazo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yetu,"alisema Mpina
Aidha aliziomba familia za wakristo kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira kwani bila kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata nafasi katika jamii.

"Familia za Kikristo lazima  ziwe mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira, hizi faini tunazowapiga watu kutokana na ukiukwaji wa sheria za mazingira kwa uchafuzi  wa Mazingira, sio kama tunawaonea bali kuwakumbusha wajibu wao "alisema
Kwa Upande wake,Mchungaji wa Kanisa la Assembly of God , Deusi Sabuni alisema  watahakikisha wanaendele kufanya Maombi kuiombea serikali ya awamu ya tano na viongozi wake.

Alisema roho za uadui zilizopo na watu kusema vibaya na kuwakatisha tamaa kusiwavunje mioyo kwa kusikiliza  maneno ya watu katika kuleta maendeleo ya nchi kwa manufaa ya taifahili na watu wake.

"Makanisa na Misikiti tupo pamoja nanyi katika kuwaombea na kama serikali hii ikiendelea hivi ndani ya miaka mitatu nchi yetu itabadilika,"alisema Mch.Sabuni.

Ibada maalum ya Kuliombea Taifa, kusifu pamoja na kuimba, ilienda sambamba na uzinduzi wa Ablum ya nyimbo za injili za mwimbaji Alfonsina Samweli pamoja na mnadawa kuuza DVDs zenye nyimbo za injili.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina akikata Utepe katika CD kuashiria kuzinduliwa kwa Abum ya Nyimbo za Injili za mwimbaji Alfonsina Samweli.


Mwimbaji Alfonsina Samweli wa kanisa la Assemblies of God la Kinziga Salasala Jijini Dar es Salaam akimpa Mkono Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, baada ya kumkabidhi kablasha lenye DVDs zenye nyimbo za Injili wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa.

Sehemu ya waumini wa kanisa la assemblies of God la Salasala. Wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga  Mpina Hayupo Pichani wakati wa ibada maalumu ya kuiombea Taifa iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni