Jumatatu, 5 Desemba 2016

Ndugu wa 3 na wengine 2, wamefariki usiku wa leo, baada ya kilabu cha pombe za kienyeji walichokuwa wakikitumia kugongwa na lori!!.

Nyumba iliyokuwa ikitumika kama kilabu ikiwa imebomoka baada ya kugongwa na lori 
lori la mizingo lenye namba za usajili T801 ACD,lililo sababisha ajali na vifo vya watu 5 

Ajali iliyo sababisha vifo vya watu 5, imetokea usiku wa leo mkoani Iringa baada ya lori la mizingo lenye namba za usajili T801 ACD lililokuwa likielekea mkoani Mbeya kuacha njia na kugonga kilabu cha pombe za kienyeji.
 

Tukio hilo limetokea majira ya saa nne kasoro usiku wa leo katika eneo la njia panda Makumbusho ya Isimila kata ya Mseke barabara kuu ya Iringa-Mbeya.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio wanasema watu hao watano wakiwemo ndugu watatu waliku ndani ya kilabu hicho wakiendelea kunywa pombe za kienyeji wakati ajali  ikitokea, mashuhuda hao wamesema lori hilo liliacha njia na ghafla lilienda kugonga nyumba ambayo ilikuwa ikitumika kama kilabu cha pombe za kienyeji na kwamba wakati ajali hiyo inatokea baadhi ya wateja walikuwa nje ya kilabu hicho hivyo waliliona lori hilo ambapo walianza kukimbia huku wakipiga kelele ili kuwasaidia waliopo ndani lakini hawakufanikiwa kukimbia.

Kwa mujibu wa Jeshi la polisi waliopoteza maisha ni leonard Mkendela (35), Neema Mkendela, Kamsia Mkendela wote wa familia moja na wengine ni Ester Mwalomo na Oscar Zosama (25) wote wakazi wa Isimila.

Majeruhi wa ajli hiyo Kasimu Ahmed Mambo (44), mkazi wa Kijiweni pia ni dereva wa lori hilo, Mussa Abdalah (34) mkazi wa kijiweni pia ni utingo wa lori lililopata ajali na Juma Abdalah omary Ally (40) ambae anadaiwa kuwa ndie alikuwa akiendesha lori hilo lililo sababisha ajali.


Wengine walio nusurika katika ajali hiyo ni muuzaji wa kilabu hicho ambaye wakati ajali inatokea alikuwa ameenda msalani nyumba ya jirani iliyo karibu na kilabu hicho. 
Dereva wa lori bw. Kasimu Ahmed akipelekwa wodini katika Hospital ya Rufaa mkoa wa Iringa

Majeruhi Musa Abdalah (34)ambe ni tingo wa lori lililo sababisha ajali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni