Jumatatu, 19 Desemba 2016

Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya limemuondoa madarakani mwenyekiti wake kutokana na kukosa imani nae!!!


Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya leo limefanya kikao cha kuadhimia kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ndg. Alex Julius Kinyamagoha kwa madai ya kukosa imani nae baada ya mwenyekiti huyo kuandika waraka na kuusambaza katika mitandao ya kijamii Facebook na WhatsApp .

Katika waraka huo Ndugu Alex Kinyamagoha anadaiwa kuandika waraka unaopinga mabadiliko yaliyojadiliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa sanjari na kuwakashfu mwenyekiti CCM Taifa aliemaliza muda wake madarakani Ndg, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mwenyekiti CCM Taifa aliyopo madarakani sasa Mh. Rais John Pombe Magufuli na kuusambaza katika mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wake wa Facebook na Whatsapp mnano tarehe 15/12/2016.

Akizungumza katika mkutano huo ndg. Frank Boaz ambae ni mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa amesema kuwa kitendo alichofanya Alex Kinyamagoha kinaashiria dhahiri kuwa alitumwa hivyo chama cha CCM hakiwezi kamwe kuwavumilia mamluki kwa namna yoyote kwani shirikisho litajengwa na wanachama wenye nia njema hivyo shirikisho halitasita kuwaondoa mamluki na tayari shirikisho hilo limeanza na Alex Kinyamagoha.

Naye Katibu wa Siasa na Uenezi Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya ndg. Oddo Aidan Ndunguru, amesema kuwa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya limekerwa na waraka huo na ambapo aliwataka watanzania waupuuze waraka huo na watambue kuwa waraka huo ni mawazo binafsi ya ndg Alex Kinyamagoha na si Shirikisho kwani Shirikisho halijawahi kufanya kikao cha kujadili mabadiliko yaliyo pendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Hata hivyo akatumia nafasi hiyo kuwaomba radhi viongozi wote wa CCM na ngazi zote, wanashirikisho na wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi kote nchini ambapo alisema kuwa Shirikisho hilo linaunga mkono mabadiliko yaliyojadiliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na uteuzi wa viongozi uliofanywa.

“hakuna haja ya kuendelea kuimba CCM iyena iyena wakati mapenzi yako yapo nje ya chama hivyo ni bora ukatoka ukaenda huko ambapo una mapenzi napo, lazima tutambue kuwa kama watangulizi wetu wangefanya makosa CCM isingekuwepo leo hivyo ccm haita wavumilia mamluki kwa namna yoyote ni lazima watoke”.

Nduguru akamaliza kwa kusema nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya juu Mkoa wa Mbeya itakaimiwa na Ndg. Michael Malegesi hadi hapo uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo utakapo fanyika, na kwamba shughuli zote za Shirikisho zitaendelea kama kawaida.

Ikumbukwe kuwa Ndg. Alex Kinyamagoha aliandika waraka huo na kuusambaza katika mitandao ya kijamii Facebook kupitia ukurasa wake na WhasApp mnamo tarehe 15/12/2016, na manamo tarehe 16/12/2016 majira ya 11:51 usiku akaomba radhi kwa waraka huo katika mtandao wa kijamii wa facebook kupitia ukurasa wake uliosomeka kama ifuatavyo...



Aliekuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya.

Katibu wa Siasa na Uenezi Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya ndg. Oddo Aidan Ndunguru.

Frank Boaz Mjumbe akizungumza katika mkutano huo.

Michael Malegesi Kaimu Mwenyekiti Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, akizungumza katika mkutano huo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni