Picha ikionesha hali ya halisi ya zoezi la bomoa bomoa linavyo tekelezwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam
Mvutano Mkali umeibuka juu ya zoezi la ubomoaji wa nyumba71,
kufuatia uongozi wa Mamlaka ya Mji Kyela kulalamikia hatua za kibabe za Halmashauri
ya Wilaya hiyo kuendesha zoezi hilo bila kuwashirikisha wakatiwakijua fika kuwa
sio eneo lao la utawala.
Halmashauri ya Wilaya inatarajia kuendesha zoezi la kubomoa
nyumba71 katika vitongoji vya Butengule na Busikali katika kata ya Nkuyu kwa
madai kuwa wahusika wamevamia eneo la hifadhi ya mbuga ya kilimo cha zao la
mpunga yaTenende.
Wakati Halmashauri ya Wilaya ikisisitiza kuwa itatekeleza zoezi
hilo kwa kuwa muda wa notisi ya siku 30 umemalizika na wavamizi hao wameshindwa
kubomoa kwa hiari yao baada ya nyumba zao kuwekwa alama ya X,
Uongoziwa wa Mamlaka ya Mji Kyela umesema zoezi hilo
halitafanyika. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya wananchi wa kata hiyo
kuandamana hadi ofisi za Mamlaka hiyo, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji
Kyela,Josephat Longoli, alisema kuwa, zoezi hilo ni batili na kwamba
Halmashauri imekiuka taratibu.
Aliongeza kuwa, uamuzi huo wa kubomoa nyumba hizo bila wao kushirikishwa
unakiuka sheria namba saba ya mwaka 1982 ya uundwaji wa serikali za mitaa na
tawala za mikoa ambayo kimsingi imetenganisha namna kila mamlaka inavyoweza
kujitawala na kuendesha shughuli zake bila kuingiliwa na mamlakanyingine.
“Suala hili nimelifikisha ofisi ya DC ‘Mkuu wa Wilaya’ ili aweze
kuliangalia upya maana licha ya Halmashauri kukiuka taratibu na kutuingilia,
lakini ile mbuga ambayo wanadai imevamiwa haimilikiwi na serikali,bali ni
mashamba ya watu na sisi tuliona tumege sehemu na kupima viwanja ilikuendeleza
mamlaka yetu” alifafanua Longoli.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Benard Semwaiko,
akifafanua juu ya suala hilo, alisema kwa mujibu wa ramani ya matumizi ya ardhi
kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaonesha kuwa,
eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya shughuliza kilimo.
“Baada ya timu ya wakuu wa idara kutembelea eneo hilo wamejiridhisha
kuwa, matumizi ya eneo hilo ni kilimo cha mpunga na kama umefika eneo hilo
utaona liko bondeni na niseme tu sisi tutaendelea na mpango wetu wakubomoa kwa
sababu tunafanya kisheria” alisema Semwaiko”.
Kuhusu suala la nyumba nane kati ya hizo 71 kuwa wahusika
wanavibali vya ujenzi , Semwaiko alisema suala hilo linafanyiwa kazi na wametoa
muda kwa wale wote walio pewa vibali kupeleka nyaraka na kama watabainika
kupewa maeneo hayo kihalali utaratibu utafanyika ili haki yao isipotee.
Awali wakizungumza na waandishi wa habari, wahanga wa zoezihilo
walilalamikia hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Halmashauri kwani wao ndio waliotoa
vibali vya ujenzi baada ya wao kuuziwa eneo hilo kama viwanja.
Mmoja wa wananchi hao walio athiriwa na zoezi hilo, Rhoda Lugano,
alisema ameishi katika eneo hilo kwa muda wa miaka mitano, lakini hakuwahi
kuona kiongozi yeyote akifika eneo hilo na kuwaeleza kuwa walikuwa hapo
kimakosa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni